Friday, September 13, 2013

MWANAMKE AMCHOMA MOTO MWANAUME ALIYEMBAKA BAADA YA KUMKARIBISHA NYUMBANI KWAKE 'KUONGEA'....

Mwanamke mmoja aliyebakwa alikuwa anaact kama nataka kumsamehe mwanaume aliyembaka miezi michache iliyopita akiwa amemtishia kisu.Mwanamke huyo aliamua kumkaribisha nyumbani kwake ili wafahamiane vizuri na pia wajadiliane maamuzi kuhusu kesi yao ya ubakaji nje ya maamuzi ya mahakama.


 Habari zilizokusanywa na Reportghananews.com zinasema kuwa,mwanaume huyo alipofika tu,mwanamke (aliyebakwa) alimpa sehemu ya kukaa alafu akamwambia kwamba anaenda kumwandalia chakula,ila alikuwa na kisasi akilini mwake.


Mwanamke huyo aliyebakwa alipanga na kaka zake kumpa fundisho mbakaji huyo. Kwa msaada wa kaka zake alimmwagia mafuta ya taa mbakaji huyo na kumchoma moto.

No comments:

Post a Comment