Tuesday, September 03, 2013

MWANAMKE ASIMULIA ALIVYOTEKWA NA KUBAKWA NA KUNDI LA WANAUME KWA MIEZI 15


Mhudumu wa kike aliyegeukia uandishi wa habari amefichua mkasa wake mbaya mno wa miezi 15 akiwa ameshikiliwa mateka na magaidi wa Kisomali ambako watekaji hao walimbaka na kucheza kamari ya Kirusi huku wakiwa na bunduki kubwa ya mashambulizi.

Amanda Lindhout alikwenda kishamba kwenye taifa hilo fukara na fukivu mwaka 2008 akiwa na umri wa miaka 24 baada ya kumshawishi rafiki yake wa kiume wa zamani kuambatana naye kwenye matembezi hayo ya hatari.
Amanda na Nigel Brennan, mpigapicha wa Australia mwenye miaka 36, walitekwa nyara katika siku yao ya tatu nchini humo.

Mwandishi mmoja wa Somalia, Abdifatah Mohammed Elmi, ambaye alikuwa akifanya kazi kama mkalimani wao, pia alikamatwa, lakini akaachiwa baada ya miezi kadhaa.

Miezi 15 ya wapenzi hao katika mateka inaelezewa katika taarifa zao zote za kutisha kwenye kitabu cha Amanda, 'A House in the Sky', kitakachoingia sokoni wiki ijayo, kwa mujibu wa gazeti la the New York Post.

Brennan hakuwa na uzoefu katika ukanda wa vita na Amanda alitumia muda kidogo nchini Irak ambako aliwahi kushikiliwa mateka wakati fulani kabla.

Huko Mogadishu, aliwatisha waandishi wakongwe kwa ujasiri wake na ushamba ambao Robert Draper alimtumia baruapepe rafiki yake wa kike: "Anaelekea kujiingiza au mtu mwingine kuuawa."

Somalia, ambayo imekosa serikali kuu kwa miaka 18, ni sehemu hatari kwa wafanyakazi wa kimataifa wa kujitolea na waandishi wa habari wakikabiliwa na hatari kutekwa na kushikiliwa na watu wenye silaha hadi watakapolipiwa kiasi cha fedha kwa ajili ya kuwakomboa.

Utawala wa upande wa Magharibi unaoongozwa na Rais Hassan Sheikh Mohamud unapambana na al Shabaab na makundi mengine ya waasi, na unashikilia pungufu ya miraba michache ya mji mkuu.

Amanda na Brennan walichukuliwa mateka baada ya magaidi kunyatia hoteli yao.

Walitekwa nyara Agosti 23, 2008 wakati walipokwenda kutembelea kambi ya wakimbizi nje ya mji mkuu huo.

Walielezwa kwamba Dola za Marekani milioni 3 za fedha za fidia zinahitajika kwa wote.

Masharti hayo haraka yakawa mabaya kufuatia kupigwa na kunyimwa chakula na Amanda kubakwa na kundi la wanaume kwa zamu.

Wakihofia kwamba wanaweza kuuawa, wawili hao wakaamua kwamba fursa yao ya kupona itaimarika kama watasilimu na kuwa Waislamu.

Haraka wakatenganishwa na kuwekwa kwenye vyumba tofauti ambako mateso yakaendelea.

Nigel hakuwa na msaada wakati alipokuwa akisikia Amanda akibakwa kupitia kwenye kuta nyembamba za gereza lao.

Mmoja wa watekaji aliweka bunduki yake kubwa ya mashambulizi kwenye kichwa cha Amanda na kucheza kamari ya Kirusi, liliripoti the Post.

Mara kwa mara walihamishiwa kwenye nyumba tofauti tofauti ambako waliwapa majina tofauti.

Wawili hao waliishi katika hofu kubwa kwamba wangekabidhiwa kwa waasi wasio na huruma wa al Shabaab, ambao Marekani inadai ni tawi la al Qaeda nchini Somalia.

Amanda akapatwa na maambukizi ya minyoo kwenye uso wake, nywele zake na kucha za vidole vya miguuni wakati Nigel alipata ugonjwa wa kuhara damu.

Baada ya siku 100, Amanda alichukuliwa peke yake kwenda kwenye jangwa. Alielezwa kupiga magoti na kichwa chake kikibanwa nyuma kwa mvuto mkali wa nywele zake, kisu kilisukumwa dhidi ya koo lake.

Aliomba asiuawe na kupewa simu ya mkononi kuongea na mama yake na kuahidi mamilioni ya dola ama sivyo atauawa.

Anaandika, kwa mujibu wa the Post: "Nilitupwa kwenye uchafu, nikilia kama mnyama, kama kitu fulani kilichojeruhiwa na kutoweza kuzungumza."

Wawili hao waliopagawa walichora mpango wa kutoroka baada ya Amanda kuwa amepelekwa kwenye jangwa peke yake usiku mmoja na kulazimishwa kuomba asiuawe kwenye uchafu.

Walitoroka kupitia dirisha la bafuni na kuruka urefu wa futi 12 hadi chini na kutimua mbio huku wakipiga mayowe kwenye msikiti moja wa mahali hapo kuomba msaada.

Wananchi wa mahali hapo hawakuwa na uwezo wa kuwaokoa wawili hao kutoka kwa watekaji wao ambao walikuwa jirani nyuma yao, washikiliaji mateka hatari zaidi waliokuwa na bunduki kubwa ya maashambulizi.

Mtu mmoja katika msikiti huo alijaribu kumkabili Amanda akiwa na bunduki lakini hakuweza kufyatua risasi. Mwanamke huyo alimkumbatia Nigel kwa karibu kabisa.

Mateka hao wakapigwa kabla ya kuchukuliwa na kupelekwa kwenye nyumba ambako vyumba vilikuwa kama selo nyeusi na panya wakikimbizana ndani yake. Walielekezewa bastola na kufungwa minyororo baada ya jaribio lao la kutoroka.

Kumekuwa na madai kwamba Amanda amejifungua mtoto wa kiume aliyempa jina la Osama wakati akiwa mateka lakini hakuzungumzia hilo," limeripoti the Post.

Mwishowe, waliachiwa huru Novemba 2009 baada ya siku 460 wakiwa mateka baada ya familia zao kukusanya pamoja maelfu ya dola na kutetea maisha yao.

Muda mfupi baada ya kuachiwa kwake, alisema: "Nilipigwa na kuteswa. Ulikuwa wakati mgumu, kupita kiasi."

Nigel alichapisha kitabu cha 'Price of a Life' mwaka 2011 wakati kitabu cha Amanda kitakuwa sokoni wiki hii. Wapenzi hao wa zamani kwa sasa hawawasiliani tena.

Amanda pia alianzisha taasisi yake ya Global Enrichment Foundation wakati akiwasaidia wanawake nchini Kenya na Somalia.

No comments:

Post a Comment