Monday, September 09, 2013

MZUNGU WA AFRICAN BARRICK GOLD KORTIN KWA KUMTELEKEZA MTOTO ALIYEZAA NA MWENYEJI...

             BI ELIZABETH JOHN AMBAYE AMEZAA NA MZUNGU 
Andre akiwa na mzazi mwenzie akimsihi aondoe shauri hilo mahakamani
                Andre akiwa na mtoto wake nje ya mahakamaANDRE LAPIERRE (50) MFANYAKAZI WA MGODI WA BULHYAHULU 

 Mzungu akitoka kusikiliza shauri lake chumba cha mahakama ambapo shauri hilo lilihairishwa mpaka tar 4.10.2013 ambapo alidhaminiwa na wadhamini wawili na fedha shilingi milioni moja

Raia wa nchini Canada ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya African Barrick Gold Bulyanhulu aliyefahamika kwa jina la Andrew Lapierre (50) amefikishwa mahakama  ya mwanzo Lunguya wilayani kahama mkoani shinyanga kwa kosa la kutelekeza mtoto kinyume cha kifungu namba 166 cha sura ya 16 aliyezaa na Bi Elizabeth John.

Akisoma makosa ya mtuhumiwa, hakimu wa mahakama ya mwanzo Lunguya Derick Masaga ameiambia mahaka kuwa Andre Lapierre  mwaka jana alimpata hujauzito Elizabeth John (21) mkazi wa Kakola ambaye alizaa mtoto wa kike aliyefahamika kwa jina la Mariam Andre, na kumtelekeza muda wote bila huduma.

Mtuhumiwa  alikana kumtelekeza mtoto huyo na kuiomba mahakama hiyo iagize wakapimwe vipimo vya vinasaba (DNA) ili kubaini ukweli na vipimo vimethibitisha hilo.

No comments:

Post a Comment