Thursday, September 19, 2013

OMMY DIMPOZ "NINA MCHUMBA MUNGU AKIJALIA NITAMUOA".


Kwenye mahojiano zaidi ya ‘Sema Yote’ aka Tell it All exclusive kwa Bongo5, Ommy Dimpoz amemzungumzia mchumba wake na jinsi ambavyo anapenda kuwa na watoto wa kike kuliko wa kiume.
0bd2f5c0206b11e389a722000a9e28d6_7
“Nina mchumba, watu wengi hawajui kuhusu mahusiano yangu lakini nina mchumba na natarajia Mungu akijalia ntakuja kumuoa. Yupo nje bado anasoma. Akimaliza shule ntamuoa,” alifunguka Ommy ambaye kwa sasa yupo nchini Marekani kwenye ziara ya wiki tatu.
Swali ni Je! Mchumba huyo ni nani? Leo kupitia Instagram, ameshare picha ya msichana mrembo aitwaye Emmy na kusababisha maswali mengi kama ndiye yeye au lah.
c51d2bb2207611e39a2a22000a1fb02b_7
Emmy
“My Biggest fan in Swiss Emmy Mwarabu,” aliandika.
Katika hatua nyingine Ommy Dimpoz alisema anapenda kuja kuwa na familia ya watoto wasiozidi watatu na anapenda watoto wa kike zaidi.
“Lakini mimi napenda watoto wa kike zaidi. Basi tu automatically nimekuwa hivyo. Pengine ni kwasababu nimelelewa sana na mama yangu.”
Hata hivyo alisema hatopenda kuona wanae wanakuwa wanamuziki kama yeye.
“Kwa maisha ya muziki ninavyoyaona na jinsi ilivyo hii kazi nisingependa mwanangu afanye,” alisema.

No comments:

Post a Comment