Sunday, September 08, 2013

PICHA YA KIVAZI CHA CHUCHU CHAZUA GUMZO NI NUSU UCHI

KIGAUNI kifupi alichokitinga mwigizaji Chuchu Hans (pichani) katika uzinduzi wa filamu ya Lulu kilizua gumzo kwa mashabiki kutokana na ufupi wake.

Chuchu alikitinga kigauni hicho hivi karibuni katika Ukumbi wa Mlimani City ambapo wadau mbalimbali walianza kuibua minong’ono kuwa huenda alipokaa kwenye kiti, alikalia mwili bila kuwa na nguo.
  Baada ya paparazi wetu kupokea minong’ono hiyo kutoka kwa wambea, fasta alimfotoa picha na kumuuliza kama ni kweli amekalia kiti bila ya nguo.
“Mh! Jamani Wabongo bwana, sasa hapa tatizo ni nini? Mbona mimi naona kawaida tu, tatizo lipo wapi?” alihoji Chuchu

No comments:

Post a Comment