Tuesday, September 10, 2013

ROSE NDAUKA, BATULI, RICHIE NA SLIM OMAR WALAMBA DEAL LA KUWA MABALOZI WA SOKO LA HISA DAR ES SALAAM(DSE).

Mastaa wa filamu Swahiliwood Rose Ndauka, Yobnesh Yusuph(Batuli), Rich na Slim Omar wamechaguliwa rasmi kuwa mabalozi wa soko la hisa la Dar es salaam/Dar es salaam Stock Exchange(DSE). Kuanzia leo wanaanza kuwa mabalozi rasmi. Wasanii hawa watatokea katika matangazo ya Tv, radio, magazetini na mitandaoni, habari za uhakika tulizozipata ni kuwa mkataba walioupata ni mnono yaani pesa ndefu kwa kwenda mbele. Vile vile mkataba huo hauwabani na kazi zao nyingine zikiwemo za filamu.
Batuli, Rose Ndauka, Slim Omar na Rich
Ni jambo zuri kuona makampuni makubwa nchini yanaanza kuwathamini wasanii wetu kama wenzetu nchi za nje zilizoendelea katika sanaa kwa makampuni makubwa kuwatumia wasanii wao. Hongereni sana.

No comments:

Post a Comment