Wednesday, September 04, 2013

SIRI YAFICHUKA: KISA CHA AUNT EZEKIEL KUPIGWA CHUPA NI PENZI LA JEFF LINALOGOMBANIWA NA WAREMBO

Siri  ya  Aunt Ezekiel  kupigwa  chupa  club  na  kujeruhiwa  mkono wake imefichuka.Habari  za  uhakika  zinadai  kwamba  Aunt  alipigwa  chumba  na  mrembo  wa  kike  katika  harakati  za  kugombea  penzi  la  mwanaume...

 Mwanaume  aliyekuwa  akigombaniwa  ni  Jeff  ambaye  anadaiwa  kuwa  ni boyfriend  wa  Yvonne ( aliyempiga  aunt  chupa )..

Kutokana  na  aibu  hiyo, mastaa  kadhaa  wameongea  na  mpekuzi  kwa  nyakati  tofauti  na  kueleza  masikitiko  yao  dhidi  ya  aunt  Ezekiel  ambaye  ni  mke  wa  mtu... 

Katika  maongezi  hayo, mastaa  hao  walidai  kwamba  mambo  anayofanya  aunt  hayaendani  na  matendo  ya  mke  wa  mtu. Aunt amekuwa  ni mtu wa baa, club  na  madanguro  mengine  ya  usiku, hali  inayotia  shaka  uhai  wa  ndoa  yake. 

" Aunt  kapata mume mwelewa sana  ambaye  kakiheshimu sana  kipaji  chake  kwa  kuto-mbana.

"Cha  ajabu yeye ameanza  kufanya  mambo ya aibu  kwa kuendekeza ngono  nje  ya  ndoa  yake" alisema star mmoja wa kike aliyekataa kuwekwa wazi jina lake ..

Muigizaji mwingine wa kike ambaye hakuwa  tayari  kuchorwa  mtandaoni  alisema:
  
 "Aunt ajiangalie sana.Yeye  ni mke wa mtu kwa  sasa. Kitendo  alichokifanya kimemchafua mpaka ukweni na asipokuwa makini  atampoteza mume wake...

"Yvonne alikuwa anamlinda bwanake, mi  siwezi kumlaumu sana ila nyie wanaume ni watu wabaya sana pia"

No comments:

Post a Comment