Sunday, September 08, 2013

TAZAMA KILIKILI MUSIC TOUR 2013 NDANI YA UWANJA WA TAIFA WA KAHAMA ILIKUWA HATARI SANA

Shangwe kwa kwenda mbele kwa wakazi wa mji wa Kahama waliofurika kwa wingi ndani ya Uwanja wa Taifa wa Kahama hivi sasa.
DJ Kim akifanya yake ndani ya Uwanja wa Taifa wa Kahama jioni hii wakati wa Tamasha la Kili Music Tour 2013 "Kikwetu Kwetu".
Wakazi wa Kahama hawataki kupitwa na Tamasha la Kili Music Tour 2013,kwani wameitikia wito kwa Wingi wa ajabu.
Wadau wakiwakilisha ndani ya Uwanja wa Taifa wa Kahama jioni hii.
Nyomi la kufa mtu ndani ya Uwanja wa Taifa hivi sasa,hakuna hata kwa kupitisha mguu.
Wadau Back Stage,
Kinadada wa Kahama wakionyesha umahiri wao wa kulizungusha nyonga.Huku Zembwela na Huku Abdallah Ambua,unahisi wanazungumza nini hapa???.....sasa hii ni Mwanzo,endelea kuvuta subira kuona mambo mazuri ya Tamasha hili la Kili Music Tour 2013 "Kikwetu Kwetu" ndani ya Uwanja wa Taifa wa Kahama.
Mwanadada Lady Jay Dee akiwapagawisaha wakazi wa Kahama usiku huu waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Taifa wa Kahama usiku huu. 


Recho akiwapa kizunguzungu wakazi wa Kahama usiku huu.


Linex Sunday, naye alikuwa mmoja kati ya wasanii waliotia fora katika tamasha la muziki la Kili Music Tour 2013 lililomalizika usiku huu kwenye Uwanja wa Taifa wa Kahama.Mara akaanza kuwaomba msamaha kwa wimbo wake I'm Sorry..... 

Mkali wa RnB,Ben Pol akionyesha ukali wake stejini.

Ben Poul akiimba kwa hisia  moja ya nyimbo zake mbele ya mashabiki lukuki waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa wa Kahama. 

Izzo Biznes akiwachana vilivyo wakazi wa Kahama.

Izzo Business na Barnaba wakiimba pamoja katika jukwaa la muziki la Kili juzi wilayani Kahama 

Mkali wa Hip Hop,Kala Jeremiah akiwapa shangwe wakazi wa Kahama.

Kala jeremiah nae hakuwa nyuma kuhakikisha kama wote wanafagilia show
Muite Ngosha the Swagger Don a.k.a Fid Q akifanya yake stejini.

Huku Ngosha na huku Izzo,unadhani nini kinaendelea hapo?

Fid Q akionyesha ujuzi wake stajeni


Roma Mkatoliki

Barnaba akimpa Ben poul zawadi ya kiatu kimoja cha kike

Lady jay dee,Ben poul,Fd Q Ngosha Ngosha,Linex,Barnaba boy katika jukwaa moja wakifanya yao
Mara ukaimbwa wimbo wa hepi besdei ya Ben Pol ambao uliwashirikisha wasanii kibao wakiepo hao waliopo jukwaani. 

nani kakwambia kuwa Kahama hakuna wanawake nyonga??

Binti wa Kahama akifanya yake stejini. 

Kahama ilikuwa ni Shangwe tupu. 

Wadau wakishow love mbele ya Bonge la Kamera. 

Kutoka kushoto ni Izzo,Lady Jay Dee pamoja na Ngosha Fid Q. 

Nyuma ya Steji. 
Kama kawaida yake akiingia lazima shangwe hapa akihakikisha kama wanasema ndio

No comments:

Post a Comment