Sunday, September 01, 2013

TAZAMA BEHIND THE SCEN YA WIMBO WA MY NUMBER ONE WA DIMOND ULIO REKODIWA HUKO SOUTH AFRICA NI BALAA

Diamond platnum
Ama kwa hakika tunapoongelea mafanikio ya kitu au watu basi nilazima tukubali kuwa Dimond amepiga hatua tena kwa juhudi zake binafsi, kwani kila analolifanya linaonekana na kuzidi kumuweka mahali pazuri kisanii kila kukicha..
 Hili linajidhihirisha wazi pale ambapo tunamuona msanii huyu akizidi kumiliki mashabiki na kufanya show nyingi zisizo na idada ndani na nnje ya nchi,pia ameendelea kufanya video za maana na kujiweeka katika nafasi kubwa ya kuwa msanii anayefanya video za gharama hivi sasa.
Wa kwanza mwenye camera ndiye meneja wa Diamond anaitwa RAKII anayefuata ni Mnyama Diamond na wa mwisho ni rafiki
Mwandishi wetu wa thesuperstarstz alibahatika kuongea nae maeneo ya sinza mori ambapo msanii huyo alisema kuwa kwasasa yeye anahitaji kuufanya mziki wa tanzania kufika mbali na pia kufungua mipaka kwa wasanii wangine kuvuka walipo ili kuleta chachu ya muziki wetu kimataifa zaidi.
Pia ametoa ushauri kwa wasaniii wengine kuwa waanze kuufanya muziki wetu kuwa wakibiashara zaidi ili kuleta mafanikio ya muziki na wao wenyewe.
Hebu tazama hii Behind the scen hii wakati Dimond akirekodi video yake huko South Africa ndipo utakapo kubaliana na mm kuwa kijana anataisha sasa

Thesuperstartz inakutakia kila la kheri na tunaku ahidi kuwa bega kwa bega na wewe katika kutimiza malengo ya muziki na wanamuziki wa africa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment