Saturday, September 14, 2013

UWOYA AJIBU MAPIGO KWA SHIGONGO

Ukurasa wa mbele wa gazeti la Risasi la leo Jumamosi (Sept 14) umetawaliwa na habari inayomhusu msanii wa Bongo Movie Irene Uwoya yenye kichwa cha habari “UWOYA MBARONI KWA WIZI WA SIMU!!”

 Katika kujibu tuhuma zilizoripotiwa na gazeti hilo, Uwoya kupitia akaunti yake ya Instagram leo amepost picha ya ukurasa wa mbele wa gazeti hilo wenye habari hiyo pamoja na maneno yafuatayo":“Mi ni mti wenye matunda milele siogop kupigwa mawe…shigongo kamua kunichafua coz nakesi nae mahakaman…anadhan ntaiacha never yeye aponde anavyoweza ila mwisho wasiku sheria iatafata mkondo wake….mi na yake mengi nayajua ila ngoja ni nyamaze nisimwagiwe tindikali”

Baada ya kuliona gazeti na post hiyo ya uwoya kama ilivyo ada ya thesuprstarstz ilimuendea uwoya hewana na kumuhoji juu ya habari hiyo na kama yeye binafsi kaliona hilo gazeti au kusikia habari hiyo

Uwoya alieleza kuwa kama kawaida yake hana la kujibu ila atahakikisha ukweli unajulikana wazi na hili atadili nalo hadi mwisho kwani anajua kinachoendelea ni kumvunja nguvu mara baada ya kusimamia vyema kesi aliyomfungulia shigongo na gazeti lake 

Akipiga stori na thesuperstarstz msanii marafu hapa nchini kwa jina la chopa wa mchopanga ambae pia ni moja ya watu wa karibu na msanii huyo alisema kuwa yeye hadi sasa hajaelewa, kwahiyo hawezi kuongelea chochote hadi awe na la kusema kwa pande zote pia ametoa ushauri kuwa hamtetei uwoya ila jamii ielewe kuwa mtu aliyempa simu hiyo ndio mwenye tatizo kwani yeye kapewa alisema chopa na kuongeza sasa tuache tuone mimi bado nalifuatilia nitakujulisha kitakachojiri kiongozi baada ya kuwa na uhakika alimaliza kusema chopa na kukata simu.

No comments:

Post a Comment