Thursday, September 05, 2013

WAKILI MAGESA AFARIKI DUNIA GHAFLA WAKATI AKISHUKA KWENYE GARI KWENDA OFISINI..!!

http://www.habarileo.co.tz/images/phares-Magesa.jpg
WAKILI wa kujitegemea wa Kampuni ya Magesa & Company Advocates, Israel Magesa, amefariki ghafla jana wakati akiteremka kwenye gari alilokuwa akiliendesha.
Akizungumza na gazeti hili kwa simu jana, mtoto wake, Phares Magesa, alisema baba yake alianguka ghafla akiwa anateremka kwenye gari na baada ya kukimbizwa hospitali ilibainika ameshafariki.

Phares alisema baba yake jana asubuhi alitoka nyumbani kama ilivyo kawaida kwenda ofisini kwake, akiwa anaendesha gari yake mwenyewe kabla ya kukutwa na umauti huo saa moja asubuhi.
Alikuwa ameshafika kazini lakini wakati anateremka kwenye gari, alianguka ghafla, alichukuliwa na kukimbizwa hospitali lakini alipofikishwa alikuwa tayari amefariki,” alisema Phares.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Ukonga Majumba Sita, ambako taratibu za mazishi zinaendelea. Mpaka sasa kwa mujibu wa Phares, familia imekubaliana Magesa aagwe Ijumaa jijini Dar es Salaam.
Baada ya hapo atasafirishwa kwenda kijiji cha Chitare, Majita, Musoma Vijijini mkoani Mara ambako maziko yatafanyika.
Tunatarajia ataagwa nyumbani na kanisani, lakini pia alikuwa ni wakili, hivyo pia kunaweza kuwa na utaratibu mwingine kutoka kwa mawakili wenzake ambao watakuwa wameuandaa,” alisema Phares.

No comments:

Post a Comment