Thursday, September 26, 2013

WANAFUNZI WA CHUO WAJIPIGA PICHA CHAFU WAKILA URODA NA KUZISAMBAZA MTANDAONI...!!HAKIKA wazazi wanaosomesha mabinti lazima wataumia wakisoma kisa hiki kilichojaa ufuska wa kutisha, Amani linakupa kwa undani.
 
Mwanafunzi wa kike aliyetajwa kwa jina moja la Agness, hivi karibuni alijifungia chumbani na njemba mmoja aitwaye Colvin na kufanya ngono zembe huku wakijirekodi na kujipiga picha za video wakidai ni kumbumbu yao.
 
Kisa hicho kinachoumiza kwa wazazi wanaolipa karo ili watoto wao wasome, kimetokea Kiwalani jijini Dar baada ya mwanafunzi huyo anayedaiwa kusoma chuo kimoja jijini humo kukacha masomo.
 
Inadaiwa kuwa binti huyo aliaga kwa wazazi wake kwamba anakwenda chuoni lakini hakufika na kukutana na mpenzi wake huyo na kujifungia chumbani.

Wakiwa chumbani kwa siku nzima wakifanya vitendo vingi vichafu ambavyo si rahisi kuviandika , hatimaye picha za video walizokuwa wakijirekodi zilivuja na kutufikia.

Mwandishi wetu alianza kufanya utafiti na hatimaye kupata habari za Colvin ambaye inadaiwa kuwa ni mchezo wake kuwarekodi wanawake anaokuwa nao faragha.
 

 “Huyu jamaa amezidi, tumemuonya mara kadhaa lakini amekuwa mgumu, anawadhalilisha wanafunzi na wake za watu wakati mwingine bila ya wao kujua kama anawarekodi,” alisema mmoja wa watu wanaomfahamu kijana huyo.

Baada ya kupata habari hizo, mwandishi wetu aliwatafuta wahusika wanaoonekana katika video hiyo ili kutaka kujua sababu ya kufanya hivyo.

Colvin ambaye ndiye mtuhumiwa namba moja wa uchafu huo, alikuwa wa kwanza kuulizwa. Hata hivyo, alijibu kwa jeuri kwa madai kuwa haoni ubaya wa kufanya jambo hilo kwani Agness ni mpenzi wake wa muda mrefu.
 

 “Ni kweli nilifanya hivyo, Agness ni mpenzi wangu, nimezaa naye, hivyo sioni ubaya kufanya mapenzi na mzazi mwenzangu huku tukijirekodi kama kumbukumbu yetu,” alisema Colvin na kukata simu huku akimtaka mwandishi wetu kutomfuatilia. 

Kwa upande wake, Agness awali alijaribu kutaka kumhonga mwandishi wetu fedha ili asichapishe picha hizo.
 
“Basi nikutumie hela usitoe hiyo habari na je, tukutane wapi ili nikupe hiyo hela…?” ilisomeka meseji ya Agness.

Msichana huyo alipoona kuna ugumu wa suala hilo kutimia akabadili maneno na kusema:
 

“Kwani kuna ubaya gani kujirekodi tukifanya mapenzi na mwandani wangu? Kama amekuwa akifanya hivyo kwa wanawake wengine miye sijali,” alisema Agness.
 
Kama vile haitoshi, Agness akaanza kutukana matusi mazito kwa mwandishi wetu ambayo hayaandikiki.

No comments:

Post a Comment