Tuesday, September 17, 2013

WOLPER MREMBO MWENYE SWAGA ZA PEKE YAKE NA ASIYEOGOPA GHARAMA TAZAMA PICHA HAPAUchunguzi wa thesuperstarstz umegundua kuwa jacklini wolper ndio mwanamke pekee ambaye hata avae nini anapendeza haya yamejidhihisha baada ya kumfuatilia kwa karibu msanii huyo ambaye anaongoza tanzania kwa wasanii wa kike katika swala la kubadili mitindo ya nywele na kuvaa huku akiwa anazidi kutoka bomba kila kukicha.

Mwanzoni mwa mwaka huu mtandao huu uliwashirikisha watu kadhaa wanaohusika na mavazi na pia watu wa make up bila kusahau salooni na kumtaja wolper kama msanii wa kike anayeongoza kufanya shoping za gharama,,,,Kiukweli mimi hapa dukani kwangu jack akija huwa sherehe yaani anaweza nunua vitu hadi vya milioni mbili alisema dada nayraty wa mlimani city nae mama hilda alisema yeye akimuona wolper anapaki gari basi ujue kwake sherehe maana ni kati ya wateja wake wakubwa..

Mdaku wetu ambaye hapendi kupitwa na habari alitinga nyumbani kwa wolper na kuambiwa ametoka na alipopewa namba yake alimjibu kuwa yupo busy kidogo na baada ya muda wolper alipiga simu ya muandishi wetu jambo ambalo muandishi wetu alilitaja kama la kiungwana maana wengine ukisha waambia we muandishi akikata simu anazima kabisa.

Mwanadada huyo anaeongoza kwa swaga alikiri kuwa yeye anafanya shoping ya gharama sana kulingana na mahitaji yake binafsi,pia alisema msanii anatakiwa apendeze na avutie sana machoni mwa watu aliongeza kuwa kwa upande wake anamshukuru mungu kuliweza hilo kwani pia kupendeza ni gharama kubwa sana.

Kipepeo wetu wa habari hizi alizidi kudodosa mrembo huyo kwakutaka kujua....Hivi .kwanini huwa unakata nywele zako na kuzifanya kuwa nyeupe au ni katika swala la kukwepa gharama?....

Msanii huyo alicheka sana na kujibu kuwa... Hii ni staili na pia ina gharama zake hadi kuwa vile na pia ni moja ya staili zangu kama nilivyotangulia kusema msanii anatakiwa abadilike badilike sio kuwa sehemu moja ndio maana leo wolper utanikuta na gauni refu kesho pensi keshokutwa kofia tshart na pens na baadae suruali na ukija kichwani lazima nibadili muonekano ili wewe ukiniona useme yule wolper alimaliza kusema wolper

Zifuatazo hapo chini ni picha za jack wolper tofauti tofauti akiwa na pozi mavazi ni mitindo ya nywele tofauti

Hapa kiheshima zaidi ila bado anatoka bombaHili  sio duka mdau hichi ni chumba anachohifadhi nguo zake msanii huyo

No comments:

Post a Comment