Wednesday, October 30, 2013

AZAM TV YAJA NA CHANNEL YA FILAMU ZA KITANZANIA ITAKAYORUSHA FILAMU HIZO MASAA 24.

Cameraman wa Azam Tv akiwa kazini

Kampuni ya Azam Tv inatarajiwa kuanza kurusha matangazo yake rasmi mwezi ujao huku moja ya Tv stesheni ikitarajiwa kuwa ya filamu za kitanzania  ambayo itazirushwa filamu hizo hewani kwa masaa 24. Azam Tv itakuwa ikitoa huduma ya matangazo ya Tv ya digitali kwa kutumia satelite yake ikiwa na king'amuzi chake ambacho kitakuwa na malipo ya aina moja tu. Azam Tv imepanga kuzifikia nchi mbalimbali na ba itarusha vipindi vya aina mbalimbali kwa ajili ya familia pia. Licha kwamba itakuwa na channel nyingine zipatazo 50 lakini pia itakuwa na channel zake tatu ambazo ni Azam One itakayokuwa ikirusha vipindi vya kiafrika hasa vya Kiswahili, Azam Two itayorusha vipindi vya kimataifa na vingine kutafsiriwa kwa kiswahili na Channel ya tatu itakuwa ni kwa ajili ya filamu za Kitanzania zitakazorushwa masaa 24. Kampuni hiyo tayari imejenga Studio zake mbili za kisasa eneo la Tabata jijini Dar es salaam kwa ajili ya vipindi vya mahojiano(Talk Shows).

Hii ni moja ya hatua nzuri kwa tasnia ya filamu nchini Tanzania kuzidi kupiga hatua na ni matumaini yetu wasanii na watengenezaji wa filamu watanufaika vizuri na Tv stesheni hiyo. Hongera Azam kwa uzalendo huo.


Wafanyakazi wa Azam Tv wakiwa pamoja na waandishi wa habari waliotembelea ofisi zao
chanzo swp

No comments:

Post a Comment