Thursday, October 31, 2013

BAADA YA KUSHIKWA UGONI WAPENZI WACHOMWA VISU.KISHA WATEKETEZWA KWA MOTO....

ADELINA Philimon (45) mkazi wa Kijiji cha Magamba wilayani Chunya na Wasiwasi Mwashiombo (28) mkazi wa Kijiji cha Ipoloto Wilayani Mbozi wanaodaiwa kuwa ni wapenzi wameuawa baada ya kuteketea kwa moto.
Wawili hao ambao kiumri ni sawa na mama na mtoto wake, waliteketea kwa moto baada ya nyumba waliyokuwa wamelala kuchomwa moto na mtu aliyetajwa kwa jina la Zacharia Mwingila (39) mkazi wa Tunduma wilayani Momba.
Chanzo cha mauaji hayo kimetajwa kuwa ni wivu wa kimapenzi ambapo mtuhumiwa ambaye kwa sasa anashikiliwa na polisi alifikia hatua ya kuchoma moto nyumba baada ya kumkuta mpenzi wake akiwa amelala na Wasiwasi majira ya saa tano za usiku wa Oktoba 25, mwaka huu katika Kijiji cha Magamba wilayani Chunya.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,  walisema mtuhumiwa huyo alianza kwa kuwachoma na visu wagoni wake na ndipo alipoamua kuchoma moto nyumba nzima ambayo iliwateketeza hadi kufa.
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Robert Mayala alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuisihi jamii kuacha vitendo vya kujichukulia sheria mikononi.

No comments:

Post a Comment