Wednesday, October 30, 2013

BREAKING NEWSSSSSS::MAMA MMOJA APIGWA RISASI NA POLISI KUJERUHIWA VIBAYA ARUSHA

Mama mmoja  amepigwa risasi na polisi  kujeruhiwa  vibaya  maeneo ya mapato arusha.
chanzo cha  tukio hilo kinasema kwamba mama huyo alifika maeneo hayo na kupaki gari yake akitaka kuingia bank lakini akaambiwa eneo hilo halifai kupaki gari,Mama huyo alipaki gari na kuingia bank alipotoka alikuta gari lake limetolewa upepo na ndipo vurugu ilianzaa baina yake yeye na polisi.Vurugu ilipokuwa kubwa mama huyo aliwaambia polisi kwamba wasimtishie bunduki hata yeye anayo na alipotaka kuitoa polisi wakampiga risasi.Mama huyo ni muuzaji maarufu wa madini  jijini arusha.Mama huyo amekimbizwa hospitali na yupo chumba cha upasuaji.CHANZO CLOUDS FM

No comments:

Post a Comment