Saturday, October 26, 2013

.DR CHENI AFUNGUKA KUHUSU UHUSIANO WA KIMAPENZI NA LULU

Ukaribu uliokuwepo kati ya msanii wa Filamu Tanzania Dr. Cheni na mwigizaji mwenzake Elizabeth Michael a.k.a Lulu umeibua maswali mengi sana kwa watu huku kukiwa na tetesi kuwa wawili hao ni wapenzi.


kupitia Kipindi cha Hatua Tatu cha Times fm Dr. Cheni amefungukia uhusiano wake na Lulu na kusema nasikia maneno mengi mtaani watu wakinituhumu kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Lulu lakini ukweli ni kwamba hakuna kinachoendelea kati yatu zaidi ya kuwa mstari wa mbele kumsaidia alipopatwa na matatizo na kuwekwa rumande kama binadamu.

Akiendelea kufunguka Cheni amesema anawashangaa watu wanaozusha mbona alishawahi kumsaidia msanii mwenzake Cloud alipopata matatizo na alikuwa mstari wa mbele kwenda polisi,kumpelekea chakula n.k lakini hakuna aliyesema lolote kwamba atakuwa na mahusiano na dada wa Cloud au nini iweje kwa Lulu wazungumze!

No comments:

Post a Comment