Thursday, October 17, 2013

HIVI NDIVYO MSANII DIAMOND ALIVYOPAGAWA MARA BAADA YA KUKUTA PICHA YAKE IMEBANDIKWA KWENYE HOTEL MAARUFU HUKO HONG KONG..!!

WABONGO walisema nabii asifiwi kwao, hicho ndicho kilichomtokea msanii wa muziki wa bongo fleva Nassib Abdul, maarufu kwa jina la Diamond Platnamz ambae yuko Hong Kong kwa sasa, msanii huyo amejikuta akipagwa kwa furaha baada ya kukuta picha yake ikiwa imebandikikwa katika moja ya kuta za Hoteli ya kitali nchini humo.
Diamond akisaini picha yake aliyoikuta ukutani
 Akiwa katika hoteli hiyo Diamond alikuta picha yake ukutani na kupagawa kwa furaha kiasi cha kuamua kutia saini katika picha hiyo, ni mara chache kwa msanii kutoka nchini Tanzania kukuta picha yake katika hotel za kifahani ndani na nje ya nchi.
Diamond amekuwa msanii mwenye mafanikio makubwa ndani na nje ya Tanzania, huku umaarufu ukienda sambamba na utajiri wa kutisha, hata hivyo msanii huyo amekumbwa na kashfa za mapenzi baada ya kuwa na tabia ya kuwachanganya watoto wa kike kila kukicha.

No comments:

Post a Comment