Thursday, October 24, 2013

INASIKITISHA SANA HILI NDILO KANISA LILILOVAMIWA NA WATU WASIOJULIKANA NA KUFANYA MAUAJI HUKO MKOANI MWANZA

Kanisa kuvamiwa na mmoja kuuwawa Mwanza October 21 2013 usiku

Mwanza ni ya mtu mmoja kuuawa na wengine watatu wamejeruhiwa kwenye shambulio lililofanywa na kundi la watu wasiofahamika usiku wa kuamkia leo ndani ya kanisa la Gilgal Christian Worship Centre Pasiansi, Ilemela Mwanza.
Tukio limetokea saa saba usiku ambapo Elia Lunyamila (35) ambaye ni mlinzi pia na mwenyekiti wa vijana wa kanisa aliuwawa akiwa amejumuika kwenye ibada na waumini wengine ambapo Alex Msakuzi na Tumsifu Pungu walijeruhiwa na hali zao sio nzuri lakini wako Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza kutokana na mapanga waliyokatwa.
Askofu wa kanisa Eliabu Sentoz alisema kama Jeshi la Polisi likiamua kukomesha hivi vitendo inawezekana kuvimaliza kabisa ambapo kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ernest Mangu amethibitisha tukio limetokea lakini mpaka sasa hakuna taarifa za kuibiwa kwa kitu chochote ndani ya kanisa kitu ambacho kinaongeza maswali zaidi kuhusu tukio lenyewe.
Waumini wakitafakari.
.


Wananchi nje ya jengo la Kanisa la Gilgal Christian Centre Pasiansi Ilemela Mwanza.
Ndugu na majirani pamoja na waumini waliomfahamu marehemu Elia Lunyamila aliyeuawa kwa kukatwa mapanga na watu wasiojulikana wakiwa wamekusanyika nyumbani kwa marehemu kuomboleza.
Askofu wa kanisa la Gilgal Christian Centre Eliabu Sentozi.

No comments:

Post a Comment