Saturday, October 12, 2013

LAZIMA NIOLEWE SIWEZI KUKAA BILA MWANAUME"....WASTARA

MWIGIZAJI mahiri Bongo, Wastara Juma Issa Abeid ‘Wastara’ amesema suala la kuolewa tena halikwepeki licha ya kutokuwa na mawazo juu ya suala hilo kwa sasa.

Akizungumza na paparazi wetu, Wastara ambaye ni nadra sana kukosea awapo mbele ya kamera, alisema yeye kama mwanamke aliyekamilika hadhani kama atakaa bila mwanaume lazima ataolewa tena.
 Mimi ni mwanamke niliyekamilika, suala la kuolewa ni lazima, japo kwa sasa sifikirii kufanya hivyo, lakini sidhani kama nitaweza kukaa bila mwanaume, lakini pia usumbufu kutoka kwao unaendelea,” alisema mwanadada huyo

Wastara ameweka wazi kuwa huko mbeleni atakaporidhia kuolewa ana amini atapata shida sana kwani bado hafikirii kama atatokea mwanaume wa kufanana na sajuki kwakila kitu,mwanadada huyo ambae hufanya maajabu awapo mbele ya camera tofauti na ukimuona amemuelezea marehemu sajuki kuwa ni mwanaume pekee alikuwa anampenda kwa dhati na hakuyumbishwa na maneno ya watu pia wastara amesema kuwa sajuki alikuwa anamridhisha kwa kila kitu.

No comments:

Post a Comment