Wednesday, October 02, 2013

MUIGIZAJI WA FILAMU HAJI ADAM(BABA HAJI) AHITIMU MASOMO YAKE YA SANAA (MAIGIZO NA FILAMU).

Muigizaji maarufu wa filamu nchini Haji Adam(Baba Haji) juzi alihitimu masomo yake ya stashahada(Diploma) kuhusiana na mambo ya maigizo na filamu kutoka chuo cha sanaa Bagamoyo. Muigizaji huyo ameongeza elimu ambayo ni rahisi kumsaidia zaidi katika kazi zake za filamu huku akiwa mmoja wa waigizaji wa siku nyingi na wenye vipaji vya kuigiza.

 Haji amecheza filamu nyingi na kazi zake mpya ni Kama Bad Luck kutoka Rj Company na nyingine mpya anashuti kwasasa akiwa na Batuli, Rose Ndauka, Slim Omar, Hashim Kambi na mastaa wengine kutoka Uganda, Kenya na Rwanda. Angalia picha za mahafali(graduation) yake yaliyofanyika Bagamoyo juzi.

Congratulation Baba Haji

No comments:

Post a Comment