Wednesday, October 16, 2013

"NISIPOFUNGA AU KUTOA PASI AMBAYO ITAPELEKEA SIMBA WAFUNGWE NITACHOMA NYUMBA ZANGU TANO NINAZOZIMILIKI"....MRISHO NGASSA


Saleh "Jembe mshambuliaji nyota wa Yanga, Mrisho Ngassa akisema kuwa hasira zake ni kama atashindwa kufunga au angalau kutoa pasi itakayozaa bao litakaloimaliza Simba: “Niko vizuri na ninajiona niko tayari kwa mchezaji, nataka kufanya kazi nzuri na ninajua Simba nitawafunga.  Kama nitashindwa kufunga basi nitatoa angalau pasi ya bao litakalosababisha Simba wafungwe. La sivyo nitachoma nyumba zangu tano ninazomiliki,” alisema Ngassa kwa kujiamini.

Yanga na Simba zinakutana Jumapili katika mechi ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment