Tuesday, October 22, 2013

SAM SHOO MKALI WA LIGHTS BONGO.

Steven Shoo

Sam Shoo mtaalam wa Lights Swahiliwood.
ANAITWA Steven Shoo ‘Sam Shoo’ kama ni mpenzi wa filamu za Bongo Movie basi jina hilo si geni katika masikio ya wapenzi wa filamu, Sam ni kiungo muhimu katika tasnia ya filamu kwani kila unapoona filamu iliyofanikiwa katika mwanga basi kijana huyu Meku amehusika, awali nilimfahamu baada ya kukutana naye katika filamu ya Danger Zone ya Ray.

.
shooo steven


Steven Shoo, Timoth Conrad

Sam Shoo akiwa na Tico
Stevee shoo 605


Steven Shoo

Sam akiwa kazini kurekebisho mwanga
Kila siku Sam anazidi kuwa mahiri katika utayarishaji wa mwanga katika filamu za kibongo na kuwa ni moja kati ya wataalamu wa mwanga (Video Lights) katika picha zetu ambazo kwa sasa zimeshika soko na kuzipotezea mbali filamu za nje kabisa, watu kama Sam kwa sasa ndio inatakiwa kuonekana umuhimu wao na hata kuongoza kulipwa vizuri.
Moja ya sifa aliyo nayo Sam ni kujituma na kupokea ushauri kwa watu mbalimbali kuhusu kazi yake ndio maana hata kuweza kuitwa kila inapotokea kazi maalum kushirikishwa kulingana na umuhimu wake katika utendaji wa kutengeneza mwanga, unapoongelea filamu bora kwa upande wa mwanga kutoka Rj Company, Kanumba Film Sam kahusika .
.
Samm Shoo 604
Steven Shoo.
Sam Shoo akiwa kazini akifunga Lights Location.
Tunapoongelea filamu bora kwa mwaka 2013/14 ya Mdundiko basi kijana Sam amehusika katika mwanga tunaona umahiri wa Sam, tupo katika kampeni ya kuwatangaza watendaji wanaofanya filamu kuwa bora na kuvutia kwa watazamaji na maendeleo ya tasnia ya filamu nasi tunakuita “SAM SHOO LIGHTS”.

No comments:

Post a Comment