Monday, October 21, 2013

TASWIRA YA MAANDALIZI YA MAZISHI YA MAREHEMU JULIUS NYAISANGAH MJINI MOROGORO.

Mbunge wa Jimbo la Morogoro Mjini, Aziz Abood ambaye ndiye mmiliki wa Kituo cha Abood Media alipokuwa akifanya kazi marehemu Nyaisangah akimpa mkono wa pole mke wa marehemu, Leah Nyaisangah nyumbani kwake Kihonda Mtaa wa Viwandani mkoani Morogoro.

Mke wa marehemu, Leah Nyaisangah akiwa na simanzi baada ya kuondokewa na mumewe.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa msibani kwa marehemu Julius Nyaisangah eneo la Kihonda Mtaa wa Viwandani mkoani Morogoro.
MAREHEMU Julius Nyaisangah 'Uncle J' aliyefariki dunia jana asubuhi baada ya kuugua kwa muda mrefu. Akizungumza na Mtandao huu, Mke wa marehemu, Leah Nyaisangah amesema kuwa mumewe alilkuwa akisumbuliwa na magonjwa ya sukari na shinikizo la damu kwa muda mrefu na amefariki jana asubuhi. Marehemu Nyaisangah mpaka mauti yanamfika alikuwa Meneja Mkuu wa Abood Media iliyopo mkoani Morogoro. Marehemu ameacha mke na watoto watatu ambao ni Samwel, Noela na Beatrice. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwa mazishi yatakayofanyika nyumbani kwao Tarime.

No comments:

Post a Comment