Thursday, October 31, 2013

Waigizaji Bongo mnaweza kujifunza kupitia hii..

Unapoamua kuwa muigizaji ili ufikishe ujumbe kwa jamii kutokana na ulichokusudia lazima uvae uhusika hasa wa kile unachokifanya.

Mara nyingi katika filamu zetu Tanzania nimeshuhudia mtu anaigiza kama ana hali ya chini lakini mavazi na muonekano wake hauendani na kile anachokifanya! Ifike kipindi tujifunze kutoka kwa wenzetu kama Nigeria ambapo mtu anapoigiza anavaa uhusika ipasavyo.

Huyu ni mmoja  wa waigizaji wa siku nyingi Nolywood,unafikiri ni nini kinamuweka kwenye chati mpaka leo? Ni uhalisia kutoka na anachokifanya..namzungumzia Mercy Johnson,hebu mcheki hapa akiwa katika matengenezo ya filamu mpya halafu jiulize wewe kama msanii unaweza hivi?

Add caption

No comments:

Post a Comment