Thursday, October 24, 2013

WASTARA AWAOMBA WADAU KUMUUNGA MKONO KATIKA SHYMAA

Msanii makali katika movie na mmiliki wa kampuni ya wajay film ameanza rasimi kurudi sokoni na mara hii amejipanga kuhakikisha hakuna pengo lolote linaloonekana.

Wastara juma kama alivyozoeleka amesema kwa sasa amejipanga kuhakikisha wajay inashusha vitu vikali na kuomba suppot ya wadau wa filamu iendelee kama zamani ili kumfanya afanye ya maana zaidi,Akizungumza na thesuperstarstz mapema hii leo wastara amesema toka mumewe afariki amekuwa katika wakati mgumu ila anamshukuru sana mungu kwakumpa moyo wa subira na sasa anarudi tena kama zamani.
Wastara ambaye alikuwa mke wa marehemu Juma kilowoko alimaarufu kama sajuki ambae alifariki na kumuacha wastara na mtoto mmoja mdogo,toka kipindi hicho wastara hajawahi  kutengeneza filamu kama yeye hadi sasa alipofanikiwa kuja na  filamu hii ambayo inaelezwa kuwa ni moto wa kuotea mbali.

Filamu hii imewashirikisha Yusuph Mlela,Salma Jabu Nisha,Wastara mwenyewe na wengine kibao ambao kwa pamoja wamefanya filamu hii kuwa moto wa  kuotea mbali,Wastara ameomba wadau kumuunga mkono katika filamu hii,,,,,Kiukweli najua hakuna filamu bila mashabiki na nina amini wadau ndio wanaoweza kuipandisha filamu hii  alisema wastara.

No comments:

Post a Comment