Tuesday, November 05, 2013

BAHATI BUKUKU APATA MSIBA MZITO WAKUFIWA NA BABA YAKE MZAZIBahati Bukuku.
MSIBA mkubwa umeikumba familia ya msanii wa nyimbo za injili, Bahati Bukuku ya baba yake mzazi Mzee Paul Bukuku kufariki dunia baada kuugua kwa muda mrefu. Marehemu amefia nyumbani kwa Bahati maeneo ya Tabata, jijini Dar es Salaam.
Akiongea na Mwandishi wetu, Bahati amethibitisha kifo cha baba yake kilichotokea asubuhi ya leo, pia amewataka Watanzania kumuombea katika kipindi hiki kigumu kwake. "Baba yangu amefariki leo baada ya kuugua kwa muda mrefu, nawaomba Watanzania waniombee kwa kipindi hiki kigumu kwangu," alisema Bahati.
THESUPERSTARSTZ INATOA POLE ZA DHATI KWA DADA BAHATI BUKUKU NA KWA FAMILIA NZIMA YA MZEE BUKUKU KWA MSIBA HUU MZITO. BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

No comments:

Post a Comment