Tuesday, November 05, 2013

BREAKING NEWS..INASIKITISHA MWANTUMU WA EXTRA BONGO AFARIKI DUNIA NA KUACHA MTOTO MDOGO

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba mcheza show wa kundi la Extra bongo marufu kwa jina la Mwantumu amefariki dunia katika hosptali ya mwananyamala alikokuwa amelazwa kwa takriban siku 4 kwa matibabu kutokana na kusumbuliwa na homa kali.
Marehemu mwantumu wa kwanza kulia anaecheka akiwa na wenzie enzi hizo
Akizungumza na thesuperstarstz muda mfupi rafiki wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Sabiha Usanga ambaye pia ni mcheza show katika alisema....Ni kweli kaka rafiki yangu Mwanatumu kafariki so hatuna jinsi tunasubiri taratibu za mazishi ila nahisi wanaweza kumsafirisha kwenda kwao kagera kwa mazishi alisema sabiha kwa masikitiko yakumpoteza rafiki yake huyo.

Marehemu alishawa kufanya kazi ndani ya bendi ya African stars twanga pepeta na hadi anafikwa na umauti alikuwa akiitumikia bendi ya Extra bongo,Mwantumu ameacha mtoto mdogo sana Mungu Ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amin.

No comments:

Post a Comment