Thursday, November 07, 2013

DEREVA ACHEZEA KICHAPO KWA KUMGONGA MTOTO MWANANYAMALA JIJINI DAR

Dereva mwenye tisheti nyekundu akipokea kichapo kutoka kwa wananchi.
Dereva akiwa hoi kwa kipigo.
Wananchi wakiwa wamelizingira daladala lililogonga mtoto.
JANA ilikuwa siku mbaya kwa dereva wa daladala lenye namba za usajili T 782 BCR linalofanya safari zake Mabibo, Mwananyamala / Makumbusho baada ya kumgonga mtoto eneo la Mwananyamala jijini Dar es Salaam.
Baada ya tukio hilo, dereva alijaribu kukimbia kutoka eneo la tukio lakini alidakwa na wananchi na kupewa kichapo cha haja. Baada ya kipondo kutoka kwa wananchi hao waliokuwa na hasira, dereva huyo alipelekwa polisi ambapo mtoto aliyegongwa alikimbizwa Hospitali ya Mwananyamala kupata matibabu.
(PICHA NA ISSA MANLLY / GPL)

No comments:

Post a Comment