Monday, November 11, 2013

Mfanyabiashara maarufu , Nickson Mushi ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi baada ya kuvamia nyumbani kwake


 Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz

--

Mfanyabiashara maarufu , Nickson Mushi, mkazi wa Msasani Maili sita mjini hapa, ameuawa kwa kupigwa risasi na  watu wanaodhaniwa kuwa majambazi baada ya kuvamia  nyumbani kwake muda mfupi baada ya kurejea kutoka katika shughuli zake.

Mushi ambaye ni mfanyabiashara  wa Mbao aliuawa na watu wasiojulikana ambao wanaaminika walitumia silaha za moto  kutekeleza uhalifu huo kisha kumkata katika maeneo ya mikono kwa kutumia panga.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio, majambazi hayo baada ya kumuua yalimpora kiasi kikubwa cha fedha zinachokadiriwa kuwa Sh. milioni 16 na 18 na  simu mbili.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz, alisema tukio hilo lilitokea juzi usiku wakati mfanyabiashara huyo akiwa na mkewe wakitoka katika shughuli zao za kazi.

Alisema wakiwa njiani wakikaribia kufika nyumbani kwao,gari moja dogo aina ya Saloon iliwapita na baadaye wakati wakikaribia getini  watu waliokuwa kwenye gari hilo walishuka na kisha kumpiga risasi na kumpora fedha.

Kamanda huyo alisema baada ya uchunguzi katika eneo la tukio kulikutwa risasi tatu, maganda mawili ya risasi na bastola moja ambayo inadaiwa kuwa ni mali ya marehemu.

Alisema polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo.Chanzo:Nipashe

No comments:

Post a Comment