Friday, November 08, 2013

KAHABA ANASWA AKIJIUZA NDANI YA GESTI HUKO SINZA..ADAIWA KUPANGA CHUMBA MAALUM KWAAJIILI YA BIASHARA HIYO...!

Zuena akiwa na mteja wake chumbani mara baada ya kunaswa na polisi.


KABANG! Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni jijini Dar kwa kushirikiana na Oparesheni    Fichua
Maovu (OFM) ya GPL wamemnasa mrembo Zuena Mohammed anayedaiwa kukodi chumba cha gesti na kuingiza wa- naume kwa zamu usiku kucha.

Zuena Mohammed akivaa nguo zake baada ya kunaswa na mteja chumbani.

Tukio hilo lilijiri chumba namba 14 ndani ya Gesti ya Mori Lodge iliyopo Sinza jijini Dar ambapo mwanamke huyo alikuwa amekodi chumba hicho na kuwapanga wanaume kwa foleni kwa ajili ya kutoa huduma haramu ya ngono.

AFM Watonywa.
Awali, ‘makachero’ wa OFM walitonywa kuwepo kwa ishu hiyo na chanzo chake kilichodai kuk- erwa na tabia ya mrembo huyo ambaye amekuwa akitishia afya za wanaume wakiwemo vigogo wa serikali ambao ilidaiwa kuwa ni sehemu ya wateja wake.
Chanzo: Jamani OFM mpo ka- zini?

...akijifunika uso kwa aibu.

OFM: Tumejaa tele leta maneno.
Chanzo: Mimi naitwa (anataja jina) lakini naomba msinitaje. Kuna mrembo mmoja amekodi chumba gesti...yaani anapanga wanaume foleni anagawa dozi ya penzi.
OFM: Hatuwezi kukutaja tuna- heshimu vyanzo vyetu vya habari. Una uhakika na taarifa zako?
Chanzo: Nina uhakika asili- mia zote. Ninyi nendeni pale Mori Lodge maeneo ya Sinza, fanyeni kazi yenu mtapata mkanda kamili.

...akiwa na polisi (kulia).
OFM kazini
Baada ya kupenyezewa ‘tipu’ hiyo, OFM iliingia kazini na ‘kuliteka’ eneo la tukio kwa uchunguzi na kubaini undani wa ufuska huo wa kutisha.
Kabla ya yote ‘memba’ wa OFM alijifanya mmoja wa wanaume waliokuwa wakihitaji huduma ya mrembo huyo hivyo kujipatia data nyingi kabla ya kubadilisha uamuzi baada ya kupata ishu kamili.

Zuena akitoka chumbani kuelekea kwenye gari la polisi.
Tukio Laivu
Kilichofuata ni kwamba OFM iliwasiliana na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kinondoni ambalo nalo baada ya kupokea taarifa hizo bila kusita lilifika eneo la tukio na kumnasa mrembo huyo akitoa hudumu kwa mwanaume ndani ya chumba hicho.
Katika hali ya sintofahamu, mazingira ndani ya chumba hicho yalionesha kuwa mrembo huyo ni mpangaji wa kudumu ambapo kulikuwa na meza ya kujiremba (dressing table) iliyosheheni mazagazaga ya vipodozi.
Ndani ya chumba hicho kulikutwa kondom zilizotumika na zisizotumika zikiwa zimezagaa sakafuni,
jambo lililothibitisha kuwepo kwa vitendo hivyo vichafu.

 
...Zuena akielekea kwenye gari la polisi.

Wanaume Watoka Nduki
Wakati mrembo huyo akinaswa, baadhi ya wanaume waliokuwa wakisubiria huduma yake walitoka nduki huku wachache wakitiwa ko- rokoroni.
Wote waliokamatwa katika sekeseke hilo walipelekwa nyuma ya nondo za Mahabusi kwenye Kituo cha Polisi Kijitonyama ‘Maba- tini’ kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Aingiza Sh. 200, 000
Chanzo chetu cha habari kilidai kuwa, kutokana na jinsi mrembo huyo ‘anavyokula vichwa’ mambo yakimuendea vizuri huweza kukusanya hadi shilingi laki mbili (200,000) kwa siku au usiku mmoja.
Baadhi ya zana alizotumia Zuena zikiwa sakafuni chumbani kwake.

No comments:

Post a Comment