Monday, November 11, 2013

NAPENDA KUMSHUKURU MUNGU KUFIKISHA MIAKA 10 YA NDOA YETU ...MKE WA JB

Mke wa kinara wa filamu hapa bongo bwana jacob stephen alimaarufu jb amezungumza na thesuperstarstz na kueleza ya moyoni kuhusu miaka kumi ya ndoa yao

Akizungumza na thesuperstarstz mke wa jb amesema kuwa kwake anamshukuru mungu sana kwakumpa maisha marefu yeye na mumewe Jacob stephen alimaarufu jb kwani kutimiza miaka kumi katika ndoa yenye furaha si jambo dogo..Kiukweli mungu ashukuriwe sana maana kutimiza miaka kumi katika ndoa yenye furaha na amani kama ilivyo kwangu na mume wangu jb alisema Irene mke wa jb.
Mwandishi wetu alipotaka kujua huwa anajisikiaje mara jb anapomuambia kuwa hatorudi anaenda kambini shemeji yetu huyo alisema,,,Kiukweli huwa ni wakati mgumu kwangu japo sina jinsi maana ni kazini kwake na ninachompendea mume wangu kama akiwa kambini muda wote napomuhitaji kuongea au kumuona sina kipingamizi hivyo kunakuwa hakuna utofauti sana kikubwana ni kuaminiana alimaliza shemeji yetu.
Baada ya kutoka kwa shemeji thesuperstarstz ilimuendea hewani Jb au bonge la bwana kama anavyopenda kuitwa na mashabiki wake alipokea na kuanza utani huku akimtania muandishi wetu,.....Haya mna habari gani tena maana nikiona simu yenu najua kuna jambo hahahaaa...Muandishi wetu alimueleza jb kuwa hakuna baya ila lengo nikukupongeza kwakutimiza miaka kumi ya ndoa yake jb alicheka sana na kusema,....Asante sana kaka ila umenishangaza umejuaje hili kaka aliuza jb huku akicheka ,kisha akaendelea kusema,,kiukweli tunamshukuru mungu sana kwa hilo kwani ndoa yetu imedumu katika furaha ya ajabu kwani kiukweli tunapendana sana sana hatujawahi kugombana wala kuchukiana maana mimi na mkewangu tumebeba vitu vitatu cha kwanza tunaishi kama mke na mume pili tunaishi kama marafiki wa ukweli na tatu tunaishi walinzi kila mtu anamlinda mwenzake kwa kumuheshimu na kwakumpenda hivyo hakutokei jambo baya dhidi yetu...alimaliza jb
Tunawapongeza sana na kuwaombea maisha marefu yenye baraka za mungu.

No comments:

Post a Comment