Saturday, November 02, 2013

NAMSHUKURU MUNGU KUTUJALIA KUPATA MTOTO WA KIKE .....WILLIAM MTITU


Jovitha Swai mke wa Mtitu akiwa na mwanae
William Mtitu

William Mtitu ambaye ni muigizaji wa filamu na producer ambaye ni mmiliki wa kampuni ya filamu ya 5Effects amefanikiwa kupata mtoto wa kike yeye na mke wake Jovitha Swai na kuwashukuru madaktari waliomsaidia mkewe kujifungua salama. Kupitia facebook Mtitu aliandika "Nawashukuru madaktari wa Hospitali ya Regency na kwa Dk. Mvungi wakiongozwa na Dk. Getu kwa kusaidia mpaka mke wangu kujifungua salama na sasa naitwa baba na mke wangu mama. Kwa kweli Mungu awabariki sana."

No comments:

Post a Comment