Sunday, November 03, 2013

NAPUMZIKA KUIGIZA MAANA FILAMU ZA KI BONGO KARIBU ZOTE ZINAFANANA...ROSE NDAUKA

Mwigizaji Rose Ndauka amesema kuwa anapumzika kwenye tasnia ya filamu kwa mwaka mmoja kwakuwa filamu za Tanzania zinafanana sana na anataka aje na kitu kipya na tofauti.

Kwa mujibu wa gazeti la mwanaspoti Rose Ndauka amesema wazo hilo limetokana na tatizo la kufanya kazi zinazojirudia mara kwa mara, hali iliyomfanya aamue kujipa likizo ya muda ili kujipanga.
Hata hivyo kauli hiyo inaweza kuwa na utata muigizaji huyo ni mjamzito kwa sasa na huenda hiyo ndio ikawa ni sababu kubwa ya yeye kusimama kwa muda.

No comments:

Post a Comment