Friday, November 29, 2013

NIKIWA KAZINI MIMI SINA ULOKOLE MUZIKI NI SEHEMU YA MAISHA YANGU.... JB

Msanii anayekimbiza hivi sasa sokoni jacob stephen alimaarufu kwa jina la jb ameeleza sababu za yeye kuendelea kuwa juu hadi sasa na kufanikiwa katika kazi zake

Akipiga story na thesuperstarstz mapema hii leo jb amesema siri kubwa ya mafanikio yake ni kujituma na pia kujifunza kila kukicha baadala ya kuona ww unajua kila kitu kumbe maisha ya sanaa ni kuigiza husika za watu,
Msanii huyo mkali amesema kwake yeye linapokuja swala la kizi uigizaji hukubali kusemwa au hata kutukanwa kwakuwa huenda kinyume na maisha yake ya kawaida..Unajua mimi ni mlokole wa damu kabisa ila linapokuja swala la kazi yangu kuna wakati ulokole naweka pembeni kwani hulazimika kwenda club kushuti au kujifunza jambo flani na mara nyingine hulazimika kuigiza kama mwanaume muhuni hii yote nikutokana na kazi yangu japo jamii yenye imani kama yangu wanakuwa wagumu kunielewa alisema jb.

Akitolea mfano movie zake jb anasema zote hufanya kwanza reseach kabla hajaicheza na ndio maana hupata mafanikio makubwa ndani na nnje ya nchi,pia jb aliendelea kusema yeye kwake sio ajabu kuandikwa vibaya au kwa zuri maana ndio kazi ya waandishi hivyo ameioma jamii kukubaliana na yeye haswa pale watakapoona jb amesemwa kwa baya wasikimbilie kukubali na kuanza kutukana au kukandia bila kujua ukweli wa jambo lenyewe.

Msanii huyu mkali wa movie ya swahiba amesema watanzania na wadau wake popote pale walipo wakae tayari kwa filamu zake nyingi ambazo hazijatoka,huku akitolea ufafanuzi filamu yake ya mikono salama aliyomshirikisha joket kwa mara ya kwanza katika filam zake..Kusema kweli napokea simu nyingi sana wadau wakitaka kujua filamu ya mikono salama itatoka lini kifupi ni kwamba ninafilamu nyingine ambazo zilitangulia kutengenezwa so lazima zitoke kwanza alafu ile itafuata nafikiri mwanzoni mwa mwezi wa nne kama hapatakuwa na mabadiliko alimaza jb ama mtumishi wa mungu kama wengi wanavyomuita.

Alipohojiwa anachokipenda jb alisema anapenda sana muziki na ndio maana muziki ukipigwa au akisikia sauti ya muziki anachanganyikiwa na hujikuta akicheza hata kama hajalipwa.

No comments:

Post a Comment