Sunday, December 01, 2013

FUNGENI MIDOMO YENU MIMI NITABAKI KUWA MIMI NA SIO NYINYI..MASOGANGE

Mwanadada mkali ambaye pia ni muuz nyago katika video mbali mbali  ndani ya bongo anayefahamika zaidi kwa jina la Agnes au Masogange amepiga stori na thesuperstarstz nakuweka wazi juu ya maswali mengi ya wadau wanauliza kila siku juu yake.

Mkali huyu amefunguka na kusema anashangazwa na watu wanaokaa na kuacha kufanya yao katika maisha na kuanza kumfuatilia au kukaa na kumongelea yeye kitu ambacho anakiona kwake sio sawa kwani kila mtu anatakiwa afanye yake na sio kumfuatilia au kumsema mtu.

Msogange ameyasema hayo huku akionyesha wazi kukerwa na watu hao ambayo amesema kwake yeye hawamuumizi kichwa kwani wao sio kamasi kwamba wakimpenga atapata tabu..Unajua nawashangaa sana binadamu hawa wasiokuwa na lakufanya kazi kila siku kukaa na kumsema Agness yaani kilanachofanya lazima wao wakijadili sijui wanafanya kazi zao saa ngapi maskini alisema masogange

Kwa uchunguzi wa mtandao wa thesuperstarstz umebaini kuwa Agness masogange ni mmoja kati ya mastar wa kike wanaongoza kwakuandikwa sana katika mitandao iwe kwa ubaya ama kwa jema.

Mwanadada huyo amewaonya wanaomfuatilia kuwa yeye atabaki kuwa Agness na hadhani kama kuna mtu anatakiwa kuingilia maisha yake...Nawaomba watu waniache hawataniweza kwakuwa mimi ndivyo nilivyo kubadilika ni mimi mwenyewe na si wezi kuwa nyie nitabaki kuwa Agnes gerald na sio nyie.

Rafiki wa karibu na mwanadada huyo amesema yeye anaamini rafiki yake huyo ni pili pili kwa wamsemao kwani ukiona watu wanakusema sana ujue wameshindwa kufika ulipo iwe kwa mazuri au kwa mabaya ndio maana kila siku hukauki midomoni mwao alimaliza mwanadada huyo mrembo.

No comments:

Post a Comment