Thursday, December 05, 2013

LULU ASEMA ANAWAOGOPA WANAUME KAMA UKOMA SOMA ALICHOKIELEZA

Muigizaji wa tanzania Elizabeth Michael ameongea na sisi na kuweka wazi au kujibu maswali ya wadau waliokuwa wakijiuliza kila mara kuhusu binti huyu aliyeshinda katika mabint warembo ambao ni mastar wa movie.

Kwanza thesupestarstz ilitaka kujua lulu toka atoke jela maisha yake ya sasa yakoje na anaichukuliaje jamii ya leo ambayo inamtazama kama lulu mpya...Mimi nashukuru mungu kunipa afya na kunilinda na mabaya ,,pili nawashukuru mashabiki wangu kwa moyo wenu wa dhati mlionionyesha katika kipindi kigumu nilichokuwa nacho ila hamkukata tamaa mlinishika bega na kuninyanyua juu,kikubwa mimi jamii naitazama kwa jicho la mbali sana nakuwaona wote kama  ndugu zangu na marafiki zangu wa karibu sana alisema msanii huyo hatari anapokuwa mbele ya camera.


Pia tulitaka kujua uhusiano wake na Dk cheni ambaye ni mtu wake wa karibu sana sana ambapo lulu alicheka sana na kusema sio kama nacheka kwa furaha nacheka kwakuwa nashangazwa na maneno ya watu yanayoenezwa kuhusu cheni...Kiukweli katika sanaa namheshimu sana cheni kwani ndio mtu pekee aliyeniingiza katika sanaa hii hadi kufika watu kunijua pili cheni ni mtu wa karibu sana na familia yangu hivyo toka nazaliwa nakuwa nikimuona cheni kama mtu wa karibu na familia yetu so namuheshimu na yeye anajua na ndio mtu pekee akifungua mdomo kuniambia jambo hata kabla hajamaliza naacha maana ananijua toka nikiwa kichanga hadi sasa 

Mwandishi wetu alitaka kujua maisha ya lulu toka ametoka jela haswa maisha ya kimahusiano ambapo lulu alifunguka na kusema..kiukweli napata wakati mgumu sana na ninasumbuliwa sana na wanaume na wanawake wenzangu juu ya swala la mapenzi ila sikudanganyi toka nimetoka jela sijawahi kukutana na mwanaume huwezi amini hadi mwenyewe najishangaa sina hamu ya kitu kinachoitwa mapenz kwa sasa ninawaogopa wanaume kama israeli mtoa roho yaani mtu akiniaambia ananipenda sijui namuonaje alimaza lulu.

Mtandao huu wa thesupestarstz uliwasiliana na Dk kilumando nassoro na kuuliza kama kuna muingiliano wowote wa kihisia au kupoteza hisia za kufanya mapenzi anapokaa mda mrefu nae alitupa majibu akisema,,,,Kifupi hakuna kitu kama hicho japo mtu unaweza kupoteza hamu ya tendo la ndoa kutokana na kuwa mtu mwenye hofu kila mara
Kauli hiyo ilianza kutupa mwanga kwani lulu bado ni mtu mwenye hofu sana kuhusu wanaume na hata rafiki yake aliwahi kukaririwa akisema lulu amekuwa mtu wakuogopa sana wanaume toka alipokumbwa na mkasa wa kuhusishwa na kifo cha nguli wa filamu nchini tanzania marehemu steven kanumba.,,,Kiukweli lulu kabadilika hadi mimi namshangaa yaani nakuwa nae muda mwingingi sana ila katika vitu vinavyomkera ni pale anapotongozwa jaman utacheka majibu yake hadi namzuiya yaani hataki kabisa maswala ya mahusiano sijui kawaje shosti wangu alisema rafiki yake huyo.

No comments:

Post a Comment