Wednesday, December 25, 2013

MISS TANZANIA 2013 ASHEREHEKEA SIKUKUU YA CHRISTMAS PAMOJA NA WATOTO YATIMA MOROGORO

 Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa Akikabidhi zawadi waliotoa katika kituo hicho kwa Mama Mkuu wa Wa shirika la Masista wa Moyo safi wa Maria Sista Flora Chuma..
 Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa (pichani), Leo amejumuika na watoto yatima wa kituo cha Mgolole  kilichopo Bigwa nje kidogo ya Mji wa Morogoro. Mrembo huo ameungana na warembo wengine wawili , akiwemo Miss Kanda ya Mashariki Missa Elzabert Pamoja  Sabra Islam Miss Morogoro 2013 . Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa.Aliongozana na Wazazi wake pamoja na Ndugu jamaa na marafiki zake  
 Mkurugenzi wa  kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundega Akiwa na  Katibu wa Miss Tanzania Bosco Majaliwa leo awlipoongozana na Miss Tanzania 2013 Happiness Watimanywa Alipotembelea Kituo cha Kulea watoto Yatima cha Mgolole Kinachomilikiwa na Masista wa Moyo safi Wa Maria  Cha Mkoani morogoro
 Watoto wa kituo cha kulea watoto yatima cha masista wa Moyo Mtakatifu wa Maria cha Mgolele mkoani Morogoro wakiwa katika Picha ya Pamoja leo walipopata Ugeni Kutoka kwa Miss tanzania Happiness Watimanywa Aliyeambatana na wakurugenzi wa Miss tanzania Pamoja na Wazazi wake ndugu na jamaa wake wa Karibu.
 Ndugu na Marafiki wa  Miss tanzania 2013 waliomsindikaza Happiness Watimanywa  Alipotembelea kituo cha watoto yatima cha mjini Morogoro.. Mama na Mwana : Miss Tanzania 2013 Hapiness Watimanywa Kulia akiwa na mama yake mzazi  

Wazazi wa Miss Tanzania Bwana na Bibi Watimanywa katika picha pamoja na Mtoto yatima wa Kituo cha Mgolele walipomsindikiza Mtoto wao Ambaye ni miss tanzania 2013 Hapiness Watimanywa alipoenda kusherekea Sikukuu ya Chrismass pamoja na watoto hao leo ambapo amepata mapokezi mazuri kutoka kwa uongozi wa kituo hicho leo
 Miss tanzania 2013 Hapiness Watimanywa Akiwa pamoja na wadogo zake wakiwa wamewabeba watoto katika yatima wa kituo hicho leo
 

 
CHANZO : MATUKIO BLOG

No comments:

Post a Comment