Sunday, December 01, 2013

SWEBE ASEMA SOKO LA FILAMU NCHINI LIMESHUKA ADAI HAJAONA MWENYE NDOTO ZA KANUMBA BONGO MOVIES

Msanii mkongwe katika tasnia ya filamu na tamthilia hapa nchini anayefahamika kwa jina swebe ambaye alivuma sana miaka ya nyuma katika kundi la kaole lilokuwa linarusha michezo yake kupitia kituo cha ITV ameibuka na kutoa kauli nzito inayoashiria kuchukizwa na jambo hilo.

Akizungumza na kwa kirefu na muandishi wetu swebe ameiambia thesuperstarstz kuwa kwasasa soko la filamu nchini linazidi kudidimia  kwa kasi bila wahusika kuliona hilo,huku wakiona kama wamefanikiwa sana kumbe wanajidanganya...Tatizo letu kaka hatutaki kuukubali ukweli kuwa kwasasa soko limebeba mambumbu wasiojua nini wanakifanya ili kuliendeleza soko lenyewe huku wakiendelea kuwapumbaza watu kuwa soko linakuwa wakati si kweli.

Msanii huyo mkali ambaye ni rafiki mkubwa wa msanii wa bongo fleva juma kasimu  nature a.k.a kiroboto au kibra katika urafiki wao ilifikia hatua sir nature akampa majina mengi rafiki yake huyo kama ishara ya kumkubali hivyo akawa anamuita Swebe santana nunda na mengine...Swebe alisema kuwa hajamzuia mtu kufanya filamu ila tujitaidi basi kusoma au kupokea mawazo mapya ya wasomi na ikibidi tutoke nnje kama alivyokuwa anafanya ndugu yetu marehemu steven kanumba..Kaka lazima tujifunze kubadilika ili tuweze kupiga hatua maana soko letu linakufa kwa majitadai na majungu yasiyokuwa na maana,alisema swebe na kuongeza kusema ,,,,Mimi bado sijaona mwenye ndoto za kanumba marehemu alijitoa kulinusuru soko na ndio maana alivuka mipaka kuhakikisha anaipeleka mbali sanaa yetu na sio kuvuka tu na kushuti movie bali hakikisha unafanya kitu cha kuwa saidia na wengine kuvuka kama alivyofanya marehemu kanumba kwa wasanii wenzake alipokuwa anawaunganisha katika matangazo na hata movie za nnje japo wengi waliishia nusu kutokana na lugha na uwezo wao kuwa mdogo alisema santana

Swebe amesema wasanii waliopo hivi sasa ni wasanii wakuridhika na mafanikio kidogo wanayoyapata na kusahau wana deni kubwa kuhakikisha wanawawezesha watoto wao wadogo zao kuvuka kiulaini hapo baadae kwani tunakoelekea soko litakuja kuwa gumu zaidi ya hapa na kama tusipokuwa makini litakufa kabisa hivyo tunatakiwa kuhakikisha tunatafuta suppot ya wataalamu ili kunusuru soko letu jambo ambalo litasaidia hapo baadae wadogo kuona mwanga na kuuendeleza...Tatizo la msanii wa nnchii hii akishapata gari na uwezo wa kupanha upande mzima wa nyumba basi kamaliza hataki tena kuangaia mbele hili nitatizo kubwa na ndicho kitu kilikuwa kinamfanya marehemu kanumba kuhangaika aliumizwa sana na hali ya wasanii wenzake kujibweteka ila mungu hakumpangia hivyo kwani mipango yake inakamilika na mungu anamchukua,Na ndio maana nakiri kuwa sijaona mwenye jitihada za kuliinua soko kama mwenzetu aliyetangulia mbele za haki.

Alipoulizwa kuhusu makundi haya mawili Bongo movie na Taff msanii huyo alijibu kuwa kwake haoni sababu ya makundi hayo kulumbana kwani sote tunachokitafuta ni kukuza sanaa yetu pia swebe alifika mbali na kusema kuwa angekuwa na mamlaka angefuta chama kimoja wapo ya hivi viwili bila kutaja ni kipi kati ya hivyo.

No comments:

Post a Comment