Tuesday, December 03, 2013

WASANII WA MUZIKI NA MOVIE ZA KISWAHILI PATRICK BASHIZ NA MAGGIE SELUWA WAFUNGA NDOA NCHINI DENMARKPongezi ziwafikie bibi na bwana kwakuona umuhimu wakuvaa vazi la kiafrika kama ishara ya kukubali asili yenu hata kama mnaishi ulaya hongerani sana
Wasanii wa movie za kiswahili pamoja na mziki wenye makazi yao nchini norway Patrick Bashizi na Maggie Seluwa wamedhihirisha upendo wao wa kweli  uliyodumu kwa muda mrefu katika hali ya uchumba na sasa wameamua kuudhihirishia ulimwengu juu ya upendo wao kwakufunga ndoa ya kifahari iliyohudhuriwa na watu maarufu nchini denmark.

 Harusi hiyo ya kipekee ilifanyika juzi tarehe 30 mwezi November katika nchi ya denmark walipo wazazi wa maggie seluwa,huku wazazi na ndugu wa patrikwakijumuika kwa pamoja kutokea norway wanapoishi,

 

Awali akizungumza na thesuperstarstz mama wa msanii huyo wa movie kutoka norway alisema anafurahiya sana mwanae kuaanza maisha mapya...Kiukweli namshukuru mungu sana mwanangu kutimiza adhima yake yakutaka kuowa na sasa kafanikiwa kwakweli mungu ni mwema sana alisema mama patrick kwa furaha sana.

kwa upande wa maggie seluwa ambaye ana vipaji vingi vinavyomfanya aheshimike nchini norwaya amesema hana la kuongea kwasasa zaidi ya kumsukuru mungu kwakufanikisha kuwa na mtu anayempenda kwa dhati na ambaye alikuwa akiota kila siku kuja kuishi nae kama mke na mume japo wamekuwa wachumba kwa muda sasa...kaka namsukuru sana mungu kwakunipa mume ambaye alikuwa katika maisha angu siku zote kwa shida na raha kiukweli nampenda sana mume wangu na mungu atupe maisha marefu pia nawashukuru wote walioshiriki kufanikisha harusi yetu kwa namna mmoja au nyingine kwani hatuna cha kuwalipa ila mungu atasema nao kwakila aliyetumia mali au muda wake kutusuppot sisi katika harusi yetu alisema msanii huyo muigizaji,,muimbaji,,na mwanamitindo maarufu nchini norway.

Hongereni sana sana hamuachi asili vazi la kiafrika linaendelea kuhusika

Wasanii hawa kwasasa wanampango wakuwekeza tanzania katika filamu za kimataifa na wamedhamiria kuwaleta mastar wakubwa wa filamu kwaajili ya kuinua kiwanda cha filamu tanzania.

Akizungumza na mwandishi wa thesuperstarstz mapema patrick amesema kwake hana furaha aliyokue ni mkali wa movie na muziki Harusi hiyo ambayo ilikuwa anaisubiri kama kufunga ndoa na mke wake kipenzi maggie seleuwa...Kaka nadhani furaha yangu imekamilika sasa sikuwa nasubiri furaha zaidi ya hiyo namshukuru mungu tumemaliza salama na kila kitu kimeenda sawa hivyo kwasasa ahadi yangu ya kuja afrika kwaajili ya kuwekeza katika soko la movie ipo pale pale na soon nitaadha kulishughulikia ili kubadili mfumo wa movie zetu alisema patrick ambeye pia ni mchezaji na muongozaji aliyesomea na kupata cheti cha kuongozaji filamu.

Endelea kucheki picha hapa

 Shamra shamra za harusi hiyo zilihudhuriwa kwa wingi na ndugu jamaa na marafiki kutoka mabara mbali mbali ulimwenguni na kushuhudia ahadi ya wawili hao patrick Bashiz na mkewe maggie seluwa ya kuishi pamoja wakiwa ni mke na mume.

Thesuperstarstz inawatakia Kila la kheri katika maisha mapya ya ndoa na hakika mlindane na kutunzana ili kuimarisha na kuilinda ahadi yenu.

HAKIKISHA UNA LIKE PAGE  YETU

No comments:

Post a Comment