Sunday, December 01, 2013

WASTARA AONYESHA KUKERWA NA WANAOMCHAFUA SOMA ALICHOKIANDIKA FECEBOOK KIUKWELI ANATIA HURUMA

 
Msanii nyota katika kiwanda cha filamu tanzania Wastara  juma ambaye alikuwa mke wa muigizaji kinara marehemu juma kilowoko (Sajuki) ameonyesha dhahiri kuumizwa na jinsi ambavyo watu wanataka kumchafua  kwakuongea ama kuandika habari ambazo hazina uhakika juu yake bila kujua huwa zinamfanya auumie sana.

Muda mfupi uliopita mwanadada huyu ameandika ujumbe unaochoma na kuumiza katika ukursa  wake wa facebook,ujumbe ambao unaashiria maumivu ya kina
                     
SOMA UJUMBE WENYEWE HAPO CHINI

Wastara Sajuki

Unaweza ukawa umefuzu masomo lakini ukashindwa na aliyefuzu maisha tumia elimu yako kuandika vitu vya kujenga taifa na kuepuka kashfa,na usiseme ulichohadithiwa ongea unachokijua.

Maisha yanamambo mengi furaha,huzuni,mateso,masim
ango,dhuruma,kuonewa,kusemwa vibaya kukatishwa tamaa lakini bado ukisimama imara na kupigania na kupigania nafasi katika dunia kama mwanadam kamili uliyepewa nafasi na mungu wako kufanya ukipendacho

Na ukafuzu kufikia lengo,mimi ninistail kuvishwa taji kama mwanamke jasili na bado nitasimama imara kutetea haki yangu na kuonesha bado nina moyo wa paka wa kupigania kinachonistail

Jioni njemaaaaaaaaa
Unlike · · Share · about an hour ago

No comments:

Post a Comment