Wednesday, January 29, 2014

GARI ANALOTUMIA DIAMOND NI LAKWANGU: CHIEF KIUMBE

  
Mara baada ya tetesi kusambaa sana mitaani na kwenye mitandao juu ya Diamond kununua ndinga mpya mara baada ya kuonekana aki-post picha akiwa na gari hilo bila neno lolote yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 245 za Kitanzania hatimaye Chief Kiumbe amefunguka juu ya ndinga hilo.

Leo asubuhi kupitia interview na kituo flani mfanya biashara ‘Chief Kiumbe’ alifunguka na kusema kwamba gari analomiliki msanii wa bongo fleva ‘Diamond’ ni la kwake.

Huu ndio ujumbe wake Chief Kiumbe.
 
“Unajua mimi huwa sio mtu wa kuzungumza sana ila ukweli ni kwamba wasanii wengi wa hapa bongo wanatembelea magari yangu, na wala hawatoi hela yoyote,kwa mfano Diamond anamiliki gari yangu mpya ambalo nilinunua zaidi ya shilingi milioni 245 kipindi niko nje kiziara, nafanya hivi kwasababu ya upendo na pia wapo wasanii wengi tu, kuna wengine wanajitamba kwamba wamenunua ila sio kweli mimi ndio ninawapa bureee watembele hizo habari za kwamba wananunua hakuna kitu kama hicho,mimi napenda watu wafuate nyayo za Diamond naamini watafanikisha ndoto zao” – Kiumbe.
CREDIT.BAABKUBWA

No comments:

Post a Comment