Monday, January 13, 2014

HALI NI MBAYA SANA HUKO KIWALANI KUNDI LA WATOTO WA MBWAMWITU LINATISHIA MAISHA YA WATU KWA KUWAKATA MAPANGA NA KUPORA MALI

Mwenyekiti wa serikali ya Mtaa wa yombo Bwana Athuman Maembe amesema kundi la kiharamia la watoto wa Mbwamwitu linaraditibiwa na Mtoto wa Mzee Lukosi.
Kundi hili linafanya uporaji wa mali za wananchi katika eneo la Kiwalani.  
Jana majira ya jioni kundi hilo lilivamia mitaa mbalimbali na kupora watu pesa na kuwakatakata watu kwa mapanga kulipiza kisasa cha wenzao wawili ambao waliuliwa juzi na wananchi wenye hasira kali kwa kuwachoma moto.
Unaweza kudhani ni simulizi za kale,.  
Huwezi kuamini kuwa ni ndani ya Jiji la Dar es salaam ambapo wakazi wa mtaa wa Karakata hulazimika kufunga biashara zao na kujifungia majumbani mwao ili kuokoa maisha yao yasije yakalaruliwa na MBWA MWITU "WATU" wanarandaranda mitaani wakiwa na silaha za jadi (mapanga, fimbo, magongo na nondo) na kupora mali na kudhuru mwili kwa kila watakayekutana naye mida ya jioni hadi usiku wa manane.
Vijana hawa wanaotembea katika makundi ya watu wasiopungua ishirini wakikutana na raia hupora hata nguo za mwilin! Sijui serikali iko likizo ama nayo ni sehemu ya mchezo? Maana kata hii ndiyo yenye kituo kikuu cha polisi cha wilaya ya Ukonga - Sitakishari. 

No comments:

Post a Comment