Saturday, January 04, 2014

JAGUAR MSANII WA KENYA AZUA UTATA BAADA YA PICHA ZAKE 6 KUSAMBAA AKIWA KATIKA MAVAZI YA MAGEREZA HUKU AKIWA CHINI YA ULINZI

jaguar1

Picha hizi 6 zimefanya watu wengi haswa mashabiki wa muziki ndani na nnje ya kenya kutaharuki kwakuamini kuwa msanii wao kipenzi kakumbwa na msala na kwenda jela.

Maswali yalikuwa mengi na  kuzua mshtuko kwenye internet kwamba Jaguar ameshikiliwa na polisi lini na ilikuwaje hadi kwenda jela?.

Baada ya kashi kashi hiyo kuzidi jaguar aliona awaondowe mashabiki zake wasi wasi kwani ni kama watu walipagawa kuona kipenzi chao kipo jela na hawaijui sababu ndipo alipotoa jibu na Jibu lake ni kwamba msanii huyu anajiandaa kutoa kazi mpya inaitwa “Kioo”.


Thesuperstarstz ilimtafuta msanii huyo na kumuuliza kulikoni ambapo alikiri kweli kuingia jela ila si kama mtuhumiwa bali ni kwaajili ya kazi....Unajua mimi ni msanii na huwa nafanya vitu ya maisha haswa kwa watu wote ni kweli nilikuwa jela ila ni kwaajili ya kazi na si kama nilikosea kitu no ni kwasababu niliona ilikupata video nzuri ya wimbo wangu huu ni vizuri ikawa na mandhari ya jela ndio sababu iliyonifanya niende hadi  jela ambapo picha hizi unazo ziona zilipigwa na si kama kulikuwa na shida alisema jaguar


Inasemekana wafungwa wa jela hiyo walifurahi kumuona Jaguar ambaye alijichanganya pamoja nao.

jaguar3

jaguar2

jaguar4

jaguar5

No comments:

Post a Comment