Wednesday, January 15, 2014

KITUMBO CHA WEMA SEPETU CHAZIDI KUKUA, MWENYEWE ASEMA NITAMTAJA MUHUSIKA,AKIRI SASA KITUMBO HAKIFICHIKI

Ni hivi majuz tu thesuperstarstz ilifanya mahojiano mafupi na star wa kiwanda cha movies bongo Wema Sepetu  nakuonyesha wazi kuwa penzi lao na diamond limeshamiri kwa sasa hali ambayo imewaweka pabaya wasichana wa diamond akiwemo penny ambao kwa sasa penz lao limefikia hatua ya kurushiana maneno kibao machafu na kutoleana siri za ndani 
Sasa limezuka jambo lingine tena na hii ni baada ya wema ku post picha zake zinaonyesha kukua kwa tumbo lake hadi kumfanya wema kuandika post kuhusu kitumbo hicho kinahowafanya watu waamini ni mimba na huku mashabiki wakifika mbali zaidi na kudai kuwa ujamzito huo huenda ukawa wa Diamond mara baada ya kurudiana na kulala wote huko hina na malaysia ambapo walikutana wakati Msanii huyo akifanya show katika nchi hizo.
Baada ya picha mpya za wema kuanza kusambaa kwenye mitandao ya kijamii na blogs huku Wema mwenyewe akiandika katika post maneno hayo hapo chini ambayo yamezidi kuwafanya watu wanaofuatilia maisha ya mastaa wa Bongo kuamini kuwa ni lazima star huyo atakuwa mjamzito baada ya tumbo lake kuanza kukua kwa kasi. Hata hivyo wengi wameanza kujiuliza kama mimba hiyo ni ya Diamond ambaye wamerudia hivi karibuni au lah !.
 
 Kutokana na fununu na minongono kuwa mingi thesuperstarstz iliamua kumtafuta wema na kutaka kujua ni kweli ana mimba au lah na kama anayo baba wa mtoto wake ninani ili mashabiki zake waondokane na maswali ambayo bado haya majibu.....Haha ha aha aha  nyie jaman hampitwi na kitu kha!!!!! hizo ni picha tu jaman so subiri muda ukifika nitaweka wazi nini maana ya kitumbo hichi na kama ni mimba nitamuweka baba wa mtoto wangu wazi kwani nampenda sana kuliko mnavyodhani alisema wema huku akifurahi sana
 

No comments:

Post a Comment