Monday, January 13, 2014

WEMA SEPETU ASEMA DIAMOND NI WAKE..AWAITA MADEMU WA DIAMOND VIRUKA NJIA

DIAMOND-WEMA
Mwanadada diva katika kiwanda cha swahili movie wema sepetu amezungumza na thesuperstars na kuweka wazi kuwa kamwe hajutuii kumsamehe Diamond na kuwa tena  mwandani wake ambaye ni mwanamuziki wa bongo fleva.

Akizungumza kwa furaha na msisitizo kuonyesha furaha yake wema amesema ni kweli waligombana na diamond na kama kuandikwa vingi vimeandikwa ila watu wajue ni ngumu sana kukausha soda katika chupa kama hujainywa au kuimwaga ukiicha na kizipo chake haitakwisha hata mara moja alisisitiza makali huyo wa movie ambae ni nadra sana kumuona katika movie na hata maisha ya kawaida.

Muandishi wetu alitaka kujua kama kweli wema na diamond wamerudiana na hapo wema alijibu na kusema kuwa....Watu wanatakiwa kujua Naseeb ni mwanaume wangu huko kutengana ni mapito tu ambayo tulikuwa tunapitia ila kwasasa yamekwisha alisema wema

Mwanadada huyo mwenye haiba ya kupendwa na watu alizidi kusisitiza kuwa kwake yeye anautofauti mkubwa sana wa penzi lake kwa mkali huyo wa nyimba ya my number one huku akisema tusimfananishe na hao viruka njia......Unajua kuna utofauti mkubwa sana wa penzi langu kwa Naseeb mimi simpendi Diamond nampenda Naseeb hao viruka njiaa wao wanampenda Diamond kwa ajili ya umaarufu na pesa mimi sipo hivyo kama pesa ninazo nying sana kuliko hata yeye na kama ni umaarufu nyie mnajua thesuperstars sasa hao wenye umaarufu uchwara na pesa zakununua mitumba lazima wajikoshe sana kwa diamond na kujifanya wanampenda kumbe hakuna lolote alizungumza kwa hasira kuonyesha kuumizwa na hali hiyo

Pia wema alisistiza kuwa watu wakae mkao wakula kuna suprise kubwa inakuja kutoka kwake na Diamond bila kutaja ni ipi na inahusu nini

2 comments: