Friday, February 14, 2014

BOB JUNIOR NA HALIMA ALI WARUDIANA NA KUFUNGA NDOA UPYA, ASHLEY TOTO KUPUMUA SASA.


Bob Junior, Halima Ali na mtoto wao katika ndoa yao iliyofanya juzi kati
Star wa Bongofleva nchini Bob Junior amerudiana na aliyekuwa mkewe ambaye waliachana miezi kadhaa iliyopita. Bob Junior amerudiana na Halima Ali ambaye pia ni actress wa filamu Swahiliwood na kufunga ndoa upya juzi kati huku mapaparazi na bloggers wengi wakishindwa kujua kwa kuwa ndoa ilifanywa siri sana. Hata hivyo Swahiliworldplanet ilikuwa ya kwanza kupenyezewa habari za wawili hao kufunga ndoa na chanzo kimoja kilicho karibu nao.

Bob Junior, Halima Ali na mtoto wao

Baada ya kupata habari hizo ilibidi kumuuliza Bob Junior kama ni kweli amerudiana na kufunga ndoa na Halima Ali aliyetamba na filamu ya Laptop, Bob Junior ambaye inadaiwa hakutaka suala hili liwe kwenye media alijibu kwa ufupi kwa kusema "Yap true". Picha hapo juu ni Bob Junior, Halima na mtoto wao katika ndoa yao mpya iliyofungwa juzi kati.
Bob Junior na Ashley Toto wakiwa Ulaya

Wawili hao kurudiana na kufunga ndoa inaweza kuwa ahueni kwa muigizaji wa filamu/promoter Ashley Toto mwenye asili ya Kenya ambaye baada ya wawili hao kutengana katika ndoa yao ya awali miezi kadhaa iliyopita Ashley alishutumiwa na baadhi ya watu kuwa ndiye aliyeivunja ndoa hiyo kwa madai ana uhusiano wa kimapenzi na Bob Junior ingawa katika mahojiano na mtandao huu Ashley alisema yeye na Bob Junior sio wapenzi bali marafiki wa kawaida tu isitoshe yeye ni Promota na Bob Junior ni mwanamuziki.

                                                            Ashley Toto

No comments:

Post a Comment