Monday, February 10, 2014

CHEKI UKUMBI WA BUNGE LA KATIBA ULIVYOKAMILIKA ,NA UTAKABIDHIWA SIKU YA JUMATANO

Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akijaribu mojawapo ya viti vipya vilivyofungwa katika ukumbi wa Bunge tayari kwa ajiri ya Matumizi wakati wa Bunge la Katiba. Mhe. Makinda aliongoza ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Bnge kufanya ukaguzi wa mwisho kabla ukumbi huo haujakabidhiwa kwa Sekretariat ya Bunge la Katiba Jumatano wiki hii.
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda akiwa na wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge kukagua ukumbi huo.
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda, (katikati) Naibu Spika Mhe. Job Ndugai (kushoto), Katibu wa Bunge (Wa pili Kulia) na Mhe. Hamadi Rashid Mohamed Kulia wakiangalia baadhi ya maboresho yaliyofanywa katika Ukumbi wa Bunge kwa ajili ya Bunge la Katiba.
Muonekano wa Ndani ya ukumbi huo baada ya kazi ya uwekaji viti kukamilika.
Mojawapo ya viti maalum vilivyowekwea katika ukumbi huo kwa ajili ya matumizi ya watu wenye ulemavu.
 
 
Viti vyote vipya vina nembo ya taifa.
Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda pamoja na wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Bunge wakiwa katika picha ya pamoja na Wafanyakazi walioshiriki kuukarabati ukumbi wa Bunge kwa ajiri ya matumizi ya Bunge la Katiba. Picha kwa hisani ya Bunge.

No comments:

Post a Comment