Thursday, February 27, 2014

MPENZI WA ZAMANI WA ETO ASEMA ETO NI BABU AACHE KUDANGANYA


Suala la umri mkubwa kwa mshambuliaji wa Chelsea raia wa Cameroon Samuel Eto'o limechukua sura mpya baada ya mpenzi wa zamani kujitokeza na kushindilia msumari mwingine.

Kocha wa Chelsea Jose Mourinho alikaririwa na moja ya vyombo vya habari vya nchini Ufaransa akisema tatizo la timu yake ya Chelsea ni washambuliaji ambao hawatumbukii wavuni kwakuwa wana umri tofauti na ule unaofahamika akitolea mfano akisema Eto'o ana miaka 32 lakini inawezekana ana miaka mitatu zaidi ya hiyo ambayo inatajwa,japo Mourinho mwenyewe amesema suala hilo alilizungumza kiutani na mtu ambaye hajui mpira huku wakicheka lakini akashangaa kupelekwa kwenye vyombo vya habari.

Sasa kama hiyo haitoshi mpenzi wake wa zamani na mama wa mtoto wake wa kwanza Anna Barranca mwenye umri wa miaka 43 akifanya kazi ya muda kwenye store inayouza nywele anasema ana ushahidi kuwa mshambuliaji huyo ana miaka zaidi ya aliyotaja wakati anaingia barani Ulaya na anadhani hana miaka 35 ana miaka zaidi ya 39.

Anasema amezaliwa mwaka 1974 ambayo inamfanya awe ana miaka 39 kwasasa lakini hati yake ya kusafiria inaonesha kuwa ana miaka 32.

Kwa wale wanaojiuliza bifu hilo limetokea wapi kwa bibie huyo,inadaiwa kuwa Eto'o alimtelekeza na binti yake ambaye alimpata miaka 11 iliyopita na sasa akimuoa mwanamke raia wa Ivory Coast ambaye ndiko ana mapenzi moto moto.

No comments:

Post a Comment