Sunday, February 09, 2014

SARAFINA JOSEPH UP COMING STAR MWENYE VIPAJI NA MALENGO LUKUKI


SARAFINA JOSEPH MOJA YA POZI ZAKE
Unapolizungumzia soko la filamu tanzania haswa kwa ukuaji wake hutoacha kutaja changamoto na wasanii up coming wanaokuja kwa kasi katika soko letu la filamu tanzania,Nachelea kusema haya mara baada ya kubahatika kumuona mwanadada huyu mwenye malengo ya hali ya juu katika kutimiza ndoto zake za kufika hollwod kwa kufanya movie.

Sarafina joseph jina sio geni sana katika masikio au midomoni mwa watu kutokana na kuja kwa kasi sana katika anga la filamu tanzani,Ni mwanadada mwenye hamu ya mafanikio na anaongoza kwa kuwa na vipaji vingi alivyojaliwa na mungu,kwanza ni muigizaji,mwanamitindo,muimbaji na mtangazaji ambaye anaongoza kipindi cha Airtel Mimi ni Bingwa kinachoruka kila ijumaa saa moja kamili hadi saa moja na nunsu katika Television ya ITV.
HAPA AKIWA KATIKA SCENE

Ni mtoto wa nne kuzaliwa akiwa ndio mtoto wa mwisho alibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume wakati anasoma  anasema ni kati ya vitu vilivyomuumiza sana wakati ule japo alifanikiwa kuendelea na masomo yake na kumkabidhi baba wa mtoto mwanae ambaye hadi sasa anaishi na baba yake,Kuhusu elimu  alisoma katika shule za Perfect Vission na alimaliza katika shule ya green acles

Mwanamama huyu wa mtoto mmoja mwenye urembo wa asili aliwahi kuuza sura pia katika video ya wimbo wa msanii Ali Kiba Hadithi Hadithi,Nifanyeje Nikupate wimbo wa Wakali Kwanza akina Makamua na josline,pia anaonekana katika nyimbo ya Keisha na Diamond ya Nimechoka ni Mmoja wawasichana waliosheheresha video hiyo ya keisha Diamond

MWANADADA SARAFINA AKIWA KAZINI
Mbali na hivyo kashacheza movie kadhaa na tamthilia,Sarafina Joseph kama anavyojulikana anapatikana pia katika movie ya The Tax Driver in love,Brother and Sisters,Reveng after pain ,Pia mrembo huyu ameshauza nyago katika Tamthilia ya 69 record inayoyoruka clouds tv sehemu ya pili.

Mwandishi wa thesuperstarstz alipopata bahati ya kuongea nae alifafanua kuwa kwa sasa amejipanga sana na ameanza kufanya movie za kizungu kwa malengo ya kupanua wigo wa soko lake na kwakuanza kashiriki katika filamu ya The leader,strugle to the unknow chini ya Equity link production ambazo amefanya katika lugha ya kizungu tupu kwa malengo ya soko la kimataifa.

Ameimbia thesuperstarstz kuwa malengo yake ni kuwa mcheza filamu wa kimataifa zaidi na ndio maana anatarajia kujiunga na chuo nchini finland mapema mwaka huu kwa ajili ya kujifunza uigizaji na utangazaji mwanadada huyo amesema soko la filamu hapa kwetu halitakuwa kama hatutokubali kupata wawekezaji wa kutosha na sio kama ilivyo sasa pia amewaomba wasanii wakubali kusoma ili kupambana na mabadiliko ya soko lenyewe.

Wasanii anaowapenda ni monalisa na Jb kwa tanzania ila amesisitiza kuwa hana maana wengine anawachukia hapana ila wanaomvutia katika filamu japo wasanii wote kwake ni ndugu na anawapenda sana.

No comments:

Post a Comment